Afisa Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Julius Kimaro akizungunza n Madiwani juu ya kumtumia mkaguzi wa ndani kufuatilia taarifa ya kamati ya Baraza hill. |
NA ODACE RWIMO,NZEGA.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Baraza la Madiwani Halmashauri ya Nzega Mkoani Tabora limetumia zaidi ya masaa sita kujadili hoja iliyotokana na taarifa ya kamati ndogo ya kuchunguza mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika katika kata ya Sigili.
Awali Mwenyekiti wa kamati ndogo ya kuchunguza mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula unaotekelezwa katika kata ya Sigili Paschal Lugonda alisema kamati hiyo iliundwa baada ya baraza kuona changamoto nyingi zinazoukabili mradi huo.
Alisema kamati hiyo ilifanya kazi kwa siku tatu kuanzia tarehe 16-18 mwezi januari mwaka huu kwa kufuata hadidu rejea ambazo ni kuta kujua uelewa wa mradi kwa wananchi,kuhakiki vikundi vilivyoainishwa kwenye taarifa ya mradi sanjar na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
Alisema kamati iliingiwa na mashaka juu ya matumizi ya fedha katika vipengele vingi ambavyo ni vikao vya vijiji na mikutano ya hadhara ambayo viligharimu milioni 6.294,malipo ya posho ya mwezi kwa timu ya wilaya milioni 14 sanajari na posho ya mwezi kwa wawezeshaji mradi 8 milioni 8.718.
Baada ya baraza kupitia taarifa hiyo iliyojaa malipo mengi kwenye vipengile tofauti mvutano ukawa mkali juu ya matumizi hayo ya fedha yalivyotumika na nani mhusika ili wamuchukulie hatua za kinidhamu hali iliypolekea mjadala mzito na mvutano mkali kwa zaidi ya masaa sita.
Kutokana na taarifa hiyo diwani wa kata ya Mambali Mkama Sadick alitaka kujua kwanini timu ya uwezeshaji ilijilipa posho ya milioni 26.857 ikiwa ni pamoja na milioni 6.87 iliyotumika kutambua teknolojia ya maeneo yanayofaa kwa ajili ya maeneo ya visima.
Hali kadhalika diwani kata ya Sigili Juma Salamba akaibuka na hoja ya kwanini hashirikishwi jambo lolote linaendelea juu ya mradi huo ili hali mradi ukiwa kwenye kata yake na wanafaika wa mradi huo wakiwa wananchi waliompigia kura.
Hata hivyo diwani wa kata ua Uduka Majonas Mshingo akaliomba baraza la madiwani kufanya maamuzi magumu kufuatia na mambo yanavyoonekana kuwa ni mabaya kwenye mradi huo kwani kunaonekana kuna ubadhilifu wa fedha za umma ni vyema kuwajibisha watimishi ambao wanasimamia mradi huo.
Baada ya kuvuta ni kuvute Afisa utumisha halmasahuri ya wilaya ya Nzega Julius Kimaro akaingilia kati na kushauri baraza la madiwani kumtumia mkaguzi wa ndani ili kukagua hali ya mwenendo ya mradi huo.
Alisema kwa vile ni suala linaloguza masrahi ya wilaya yetu ni vyema tukimuagiza mkaguzi wa ndani ukauangalie mradi huo na kujirisha juu matumizi ya fedha hizo kama yanatumika kwa mjibu wa sheria ama kunaukiukwaji wa matumizi ya fedha.
Alisema ripoti ya mkaguzi wa ndani itatoa mwaga wa kutosha juu yaliyoletwa na kamati ndogo ya uchunguzi na tutakuwa na wingo mpana wa kujadili taarifa ya mkaguzi wa ndani na kuchukuwa hatua za kinidhamu na kisheria.
Kimaro alishauri kutokumsimamisha mtumishi yoyote mpaka pale taarifa ya mkaguzi wa ndani itakapobainisha matumizi mabaya yaliyofanyika kwenye mradi huo kwa kuwa yeye atapitia miongozo yote ya matumizi ya fedha za mradi na kukaguwa kwa kina kama hayajakiukwa.
Alisema kwenye miradi mingi ya serikali inakuwa ni miongozo yake hasa katika matumizi ya fedha na wapi itumike kwa kitu gani na kama mkaguzi atagungundua matumizi nje ya muongozo wa mradi itakuwa ni vyema kuchukuwa hatua zaidi kwa wahusika.
Baada ya maelezo hayo baraza la madiwani kupitia kwa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Heneriko Kanoga alimshukuru na kumupongeza Afisa huyo kwa kutumia taalamu kwa kuwaelewesha madiwani sanjali na kutoa ushauri mzuri ambao umesaidia kuondoa utata ulikuwepo.
Alisema baraza hili bila wewe kuingilia kati na kutoa muongozo bora wa namna ya kufanya ungetuchukuwa masaa zaidi haya tuliyotumia kwani ki uhalisia mradi huu bado unafikilisha kwa namna unavotekelezwa na kusimamiwa.
Alisema kama kamati ilivyogundua mambo mengi ambayo kimsingi hatukayafahamu ndio maana baraza langu lilikuwa na maswali mengi ya kujiuliza na kutaka kupatiwa majibu kwa kuwa tumemua kumtumia mkaguzi wa ndani naamini atatupatia majibu sahihi.
Hata hivyo naomba madiwani tuwe ni imani juu ya mkaguzi wa ndani kuwa atatusaidia kufichua yale yaliyojificha kama alivyosema afisa wetu wa kwani siyo jambo la kulidhisha ukipitia taarifa hii inatia mashaka sana.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇