LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 4, 2023

AJALI YA GARI YAUA WATU 17,Y AJERUHI 12 MKOANI TANGA

 WATU 17 wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya magari mawili likiwemo gari iliyokuwa ikisafirisha msiba kugongana uso kwa uso usiku wa kuamkia Jumamosi Februari 4, 2023 katika eneo la Magira Gereza wilayani Korogwe mkoani Tanga.


Imeelezwa kuwa ajali hiyo imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar kwenda Moshi kwenye mazishi.

Akizungumzia ajali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesemaa wananchi wa Mkoa Wa Tanga na Tanzania kwa ujumla wamepokea kwa masikitiko makubwa tukio la ajali hiyo iliyotokea usiku wa leo ikihusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 17 na majeruhi 12 pamoja na uharibufu mkubwa wa nagari hayo.

"Ajali imetokea Februari 3,2023 , saa 4.30 usiku eneo la Magila Gereza katika Kata ya Magila Gereza Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe, Barabara Kuu ya Segera - Buiko. Magari yaliyohusika na ajali hiyo ni gari namba T 673 CUC aina Mitsubish Fuso Ikiendeshwa na Dereva ambaye jina lake halijafamika iligonga na gari T 863 DXN aina ya Coaster Coaster Iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na Abiria 26 Ikiyokea Dar es Salaam kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa mazishi.

"Ajali hii imesababisha vifo 17 na najeruhi 12 ambao majina yao wote Hayajafahamika. Miili ya narehemu imehifafhiwa katika Hospital yetu ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospital ya Mkoa wa Tanga Bombo na majeruhi 2 wamebaki Hospital ya Korogwe kwa Matibabu,"amesema Mgumba

Aidha ameeleza kwamba chanzo cha ajali ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa gari namba T 673 CUC M/Fuso Kulipita gari la mbele bila ya kuchukua tahadhari na kugongana uso kwa uso gari namba T863 DXN T/Coaster.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa bada ya magari yote yaliyopata ajali yamekaguliwa na yameshaondolewa barabarani na sasa barabara inapitika.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages