Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete amewataka watakaopewa miradi ya Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP), kuwa wazalendo na kutokuwa wachoyo wa kuwapatia ajira vijana wa kitanzania. Aidha amesema kuwa mradi huo utazalisha zaidi ya ajira 10,000 na takribani hati milki mil 2.5 zitatolewa katika maeneo ya miradi. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Steven Kiruswa.
Ameyasema hayo alipokuwa akizindua majadiliano ya mradi huo jijini Dodoma Januari 17, 2023. Ridhiwani amezidua mradi huo kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dkt Angeline Mabula.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo ya ardhi, Dkt Allan Kijazi
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Ridhiwani akifungua majadiliano, Naibu Waziri wa Madini, Kiruswa, Mkuu wa Mkoa wa Dodod, Senyamule na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mgumba wakielezea manufaa ya mradi huo...IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇