Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374.
*25 za Kata/Serikali
*2 za Binafsi
(SDA & KATOLIKI)
UPUNGUFU WA MIUNDOMBINU
Tunaendelea na ujenzi na uboreshaji wa miundombimu iliyopungufu kwenye Sekondari zetu za Kata.
Bado kuna mahitaji ya maabara, maktaba, vyumba vya madarasa, ofisi za walimu (majengo ya utawala), vyoo, nyumba za walimu, n.k. kwenye Sekondari zetu za Kata.
Vilevile, kuna matatizo ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda masomoni, na mirundikano ya wanafunzi madarasani (wingi wa watoto wanaopaswa kwenda sekondari) - tunalazimika kuongeza idadi ya sekondari kwenye baadhi ya kata zetu.
Tunashukuru sana Serikali yetu, chini ya uongozi wa Rais wetu, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, kuendelea kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombimu iliyotajwa hapo juu.
HARAMBEE ZA MBUNGE WA JIMBO
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, ataendesha HARAMBEE MBILI kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye SEKONDARI MBILI.
(1) BWAI SEKONDARI
Hii ni Sekondari mpya na ya pili ya Kata ya Kiriba ambayo imefunguliwa wiki iliyopita. Mategemeo ni kuwa na Wanafunzi 150 wa Kidato cha kwanza (Form I)
Harambee Bwai Sekondari
*Alhamisi, 19.1.2023
*Saa 9 alasiri (15 hrs)
Michango ipelekwe kwa:
*Headmaster
0757 471 516
0612 409 257
(2) MUHOJI SEKONDARI
Sekondari hii inajengwa kwenye Kata ya Bugwema yenye vijiji vinne (4), na ambayo ni kubwa (eneo) kuzidi Kata zetu zote.
Hii itakuwa Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema
Harambee Muhoji Sekondari
*Jumanne, 24.1.2023
*Saa 8 mchana (14 hrs)
Michango ipelekwe kwa:
*Mtendaji wa Kijiji (VEO)
0686 557 264
*MICHANGO inaombwa kutoka kwa Wazaliwa wa Musoma Vijijini na hasa wa kutoka maeneo yenye miradi hiyo, na Wadau wengine wa Maendeleo - KARIBUNI SANA!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumanne, 17.1.2023
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇