LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 16, 2023

RAIS DK. MWIYI ATEUA KAMISHNA MKUU ZRA KUTIMIZA MATAKWA YA KISHERIA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato zanzibar (ZRA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katiu Mkuu Kiongozi Zanzibar Mhandisi Zena Said uteuzi huo umeanza Januari 10, 2023.

"Kufuatia kufutwa kwa Sheria ya Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ya mwaka 1996 na kutungwa Sheria ya Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ya mwaka 2022, Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Ndugu Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar", imesema taarifa hiyo.

Rais Dk. Mwinyi

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages