LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 16, 2023

SOPHIA MJEMA ATINGA CCM LUMUMBA LEO, AZUNGUMZA NA WATUMISHI WAKIWEMO MAAFISA WA IDARA YAKE YA UENEZI

Na Bashir Nkoromo, Lumumba, Dar es Salaam
Katibu mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Idara ya Itikadi na Uenezi Sophia Mjema amewataka watumishi wa Chama na maafisa wa idara yake ya Itikadi na Uenezi kuchangamsha akili na weledi katika kutekeleza majukumu yao.

Mjema ambaye aliteuliwa juzi kupitia vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa vilivyofanyika juzi Ikulu Jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema hayo akizungumza na Watumishi na maafisa hao, baada ya kufika kwa mara ya kwanza ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Amewataka watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa bidii, umoja, ubunifu na kuhakikisha wakati wote wanakuwa mfano bora katika kuendelea kujenga, kutunza na kulinda haiba nzuri ya Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wake Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mjema ambaye ameteuliwa kushika nafasi hiyo mpya akiwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, amesisitiza kazi kubwa iliyopo mbele ya watumishi hao ni kuendelea kuyasema kwa wananchi mazuri yanayofanyika ili wayafahamu.

Sanjari na hilo, amewataka pia kueleza uzuri wa CCM, kusikiliza kero au changamoto walizo nazo Wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi, kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuendelea kuwajengea uwezo wanachama na viongozi kupitia mafunzo.

"Kazi zote hizi hazipaswi kusubiri, tuanze sasa na tuendelee mbele", akasisitiza Mjema .

Katibu mpya wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Sophia Mjema akisaini Kitabu baada ya kuingia kwa mara ya kwanza Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo.

Katibu mpya wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Sophia Mjema akikabidhiwa Ofisi na Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara hiyo Ndugu Zakaria Mwansasu, alipofika kwa mara ya akwanza katika Ofisi hiyo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages