LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 15, 2023

MWENYEKITI WA MACHINGA MKOA WA PWANI APONGEZA UTEKELEZAJI ILANI

 Na Dismas Lyassa, Kibaha



MWENYEKITI wa Machinga Mkoa wa Pwani ndugu Filemon Maliga na Mjumbe wa Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani ameipongeza Serikali kwa kutekelezaji Ilani ya Uchaguzi hasa upande wa kushughulikia kero za wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la machinga.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjijni Silvestry Francis Koka  (wa tano kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi baada ya mkutano wake na machinga katika soko la Mnarani 'Loliondo' Kibaha mjini.



“Nampongeza sana Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutenga bajeti ya Tsh45bilioni kwa ajili ya machinga, kwa mwaka 2022/2023 kwa ajili ya miundo mbinu na mitaji. Nampongeza pia kwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa ya kila mkoa kupata ofisi ya machinga, sisi machinga wa mkoa wa Pwani tayari tumeanza kupokea maelekezo ya ujenzi wa ofisi ya machinga mkoa,” alisema Maliga na kusisitiza kuwa wafanyabiashara wawe kwenye sehemu rasmi na kuunda vikundi ili waweze kukopesheka.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages