Na Dismas Lyassa, Kibaha
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Fransis Koka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mnarani maarufu Soko la Loliondo |
MBUNGE wa Jimbo Kibaha Mjini ndugu Silyvestry Koka leo 15/01/2023 ameshiriki Mkutano wa Wafanyabiashara wa Stendi ya Mnarani maarufu kama soko la Loliondo na kutoa maagizo ya kushughulikia kero zao hivyo kutoa furaha kwa wafanyabiashara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na ofisi ya Mbunge, ndugu Koka ameshiriki ziara hiyo kufuatia mwaliko aliopewa kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Wafanyabiashara hao wametumia Mkutano huo wa kufungua Mwaka kumtembeza ndugu Koka kwenye vitengo kadhaa vya soko hilo ili kumweleza changamoto mbalimbali sokoni hapo.
Pamoja na mambo mengine wafanyabiashara hao wamemweleza Mbunge Changamoto ya uchakavu wa Stendi ya Mnarani, changamoto ya takataka kutozolewa kwa wakati, changamoto uchakavu wa paa la soko la matunda.
Aidha Mbunge alipokea maombi ya wafanyabiashara wa chipsi kujengewa paa la bati tofauti na wanalotumia sasa la maturubai.
Akijibu changamoto hizo Mbunge Koka amemwagiza Meneja wa Soko hilo Bwana Felix Kishenyi kwa kushirikiana na Halmashauri kushughulikia changamoto hizo kwa haraka ukingazingatia kuwa Halmashauri inapata mapato sokoni hapo.
Aidha Mbunge amewaeleza wafanyabiashara hayo kuwa Halmashauri tayari imeanza mchakato wa kuiwekea rami stendi hiyo Ili kuondokana mashimo kwenye Stendi hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇