Na Dismas Lyassa, Kibaha
MWENYEKITI wa Soko la Mnarani maarufu kwa jina la Loliondo, lililoko Kibaha Mjini Mkoani Pwani, ndugu Mohammed Mnembwe amempongeza Mbunge wa jimbo hilo ndugu Sylvestry Koka kutokana na kushughulikia kero za soko hilo.
Mwenyekiti wa soko la Mnarani Mohammed Mnembwe akiteta jambo la Mbunge wa Kibaha Mjini Sylvestry Koka (kushoto) |
“Mbunge wetu amekuwa msaada mkubwa katika soko letu katika kushughulikia kero za wafanyabiashara, hata leo sisi wafanyabiashara tulikuwa na mkutano nae wenye lengo la kuendelea kuangalia namna ya kuendelea kuboresha shughuli zetu,” alisema Mohammed na kuongeza kuwa kitendo cha Mbunge kuacha shughuli zake na kuja kutusikiliza wafanyabiashara kinaonyesha ni namna gani anatujali.
Mwenyekiti huyo amezitaja baadhi ya kero zilizoko kwenye soko hilo kuwa ni ubovu wa baa katika kitengo cha wauza matunda wa jumla na rejareja.
“Kwenye changamoto hii mbunge wetu ametuahidi kutusaidia kuezeka mapaa yote mawili, pia ameagiza stendi yote ya daladala Loliondo kuwekwa rami pamoja na maeneo ya kupumzikia abiria,” alisema mwenyekiti huyo.
Katika stendi pia kumekuwa na giza wakati wa usiku kutokana na kutokuwa na taa, mbunge Koka ameagiza taa ziwekwe mara moja.
Aidha ameagiza kufanyiwa maboresho katika kitendo cha mchele na soko lote kwa ujumla ili kusaidia kuharakisha maendeleo kwenye soko hilo muhimu kwa wajasiriamali.
Soko la Loliondo ambalo lilianzishwa 2017 lina zaidi ya wafanyabiashara 2000.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇