LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 18, 2023

HEKA-HEKA ZA MAPOKEZI YA MWENYEKITI WA UWT MARY CHATANDA MKOANI DAR ES SALAAM, JANA

 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda, akikabidhi sehemu ya msaada wa Vitu mbalimbali kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Taasisi ya Ocean Road Dk. Julius Mwaiselage, alipofika na msafara wake kwenye Hospitali hiyo, katika mapokezi aliyofanyiwa na UWT mkoa wa Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa UWT Mariam Shomari. Kulia ni Diwani wa Kivukoni Sharik Choughle, Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Adamu Ngalawa na Mwenyekiti wa UWT mkoa huo Mwajabu Mbwambo.

Zifuatazo ni picha zaidi ya 100 za taswira ya tukio hilo

Mwenyekiti Chatanda akiwa Taasisi ya Ocean Road👇





















Baada ya Ocean Road Mwenyekiti Chatanda akaenda kufanyiwa mapokezi rasmi katika Ukumbi wa Kiramuu, Mbezi Beach👇





































Makamu Mwenyekiti UWT Mariam Shomari akizungumza na maelfu ya Wana UWT ukumbini👇


Mwenyekiti Chatanda akihutubia maelfu ya Wana UWT ukumbini👇



Kamisaa wa CCM DC wa Ubungo Kheri James akiomba ruhusa yeye na wenzake waliohudhuria hafla hiyo waondoke baada ya kusikiliza hotuba ya Mwenyekiti Chatanda.
Ma DC wakiaga. Anayepeana mkono na Mwenyekiti Chatanda ni DC wa Kigamboni Fatma Nyangasa. 

Kisha Mwenyekiti akatoa kadi kwa Wanachama Wapya. Alikabidhi watano kwa niaba ya Wanachama wapya zaidi ya 400👇
Akikabidhi kadi.
Watano waliokabidhiwa kadi kwa niaba ya wenzao
Kiapo cha Mwanachama.


Halafu ikafika Hekaheka ya kumzawadia Mwenyekiti Chatanda na Makamu wake, Wakianza Kinondoni👇




Halafu shughuli ikahamia mjini katika ukumbi mdogo wa Bunge ambako Mwenyeki Chatanda aliandaliwa Keki👇👇








Mwisho Mwenyekiti Chatanda akasema "Asanteni sana UWT Dar es Salaam, kwa mapokezi makubwa mliyonipa. Kule ukumbini nilistaajabu mlivyofurika kwa wingi, sasa na hili tukio la kustukiza la keki mmezidi kunipa nguvu mno. Mimi na Makamu tunawaahidi kuchapa kazi usiku na mchana, iwe mvua au jua. Mimi simu yangu huwa sizimi tuwasiliane wakati wote. Haya ngoja niwatajie namba yangu ambaye hana aiandike....".
ENDS

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages