Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzana (UWT) Mary Chatanda, akizungumza jana.
Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Mbezi Beach
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzana (UWT) Mary Chatanda, amewapiga marufuku kuanzia jana Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum kuandaa na kufanya vikao na Wajumbe wa Baraza, na kuonya kuwa atakayekiuka marufuku hiyo atahukuliwaa hatua stahiki.
Amesema, miongoni mwa hatua atakazochukuliwa Mbunge au Diwani wa Viti Maalum akibainika kukiuka marufuku hiyo ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kufikishwa kwenye vikao kuonywa na akikaidi zaidi atafikishwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.
Chatanda alitaja hayo, akizungumza na Viongozi na Wanachama wa UWT katika Mkutano uliofanyika jana, katika Ukumbi wa Kiramuu, Mbezi Beach, Kata ya Kawe, ukiwa sehemu ya mapokezi rasmi yaliyofanywa na UWT mkoa wa Dar es Salaam, kufuatia kuwasili kwake mkoani hapa kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo.
Tafadhali msikilize Chatanda HAPO👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇