UWT imempongeza Rais Samia kwa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa uenyekitiTaifa pamoja na kupatiwa tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Rugangira akitangaza maazimio hayo 7. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, Mary Chatanda.
MAAZIMIO YA UWT TAREHE 9/12/2022
Sisi Umoja wa Wanawake Tanzania chini ya Mwenyekiti Mary Chatanda, tuliokutana leo hapa Dodoma tarehe 9/12/2022 katika Kongamano la Kumpogeza Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi, tumeazimia
1. Tunampongeza sana Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kwa Kishindo kuwa Mwenyekiti wa Sita wa Chama Cha Mapinduzi.
2. Kutokana na kazi kubwa na nzuri anazozifanya; sisi Wanawake wa Tanzania tutamsemea, tutampigania na kumpambania Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza majukumu yake na tutahakikisha Chama Cha Mapinduzi kinapata Ushindi wa Kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2024/2025.
3. Kwa kutambua kuwa Wanawake ndio nguzo ya familia, tutatimiza wajibu wetu katika malezi, makuzi, ustawi na maendeleo ya watoto na familia ikiwemo kuhakikisha tunadumisha maadili, desturi na tamadumi chanya kwa ajili ya maendeleo ya Nchi yetu'
4. Tutafanya uchambuzi na ufuatiliaji wa Bajeti ya Serikali hususan kwenye maeneo yanayolenga kuwainua wanawake na watoto.
5. Tukitambua dhamira ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwapa nafasi za Uongozi sisi Wanawake tunaahidi tutajikoteza kwa wingi kugombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
6. Tutakuwa mstari wa mbele kuwatafuta, kuwashawishi, kuwalea na kuwajengea uwezo mabinti na wanawake kugombea na kuwainua katika nafasi za Uongozi.
7. Tutapinga aina zote za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto nchini
UWT Imara….Jeshi La Mama….KaziIendelee
Imetolewa na:
Mary Pius Chatada,
Mwenyekiti UWT Taifa.
Tarehe: 9 Desemba 2022
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇