*Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374. Jumla ya Shule za Msingi za Jimboni mwetu ni 118 (shule 3 ni za Binafsi). Vilevile, tunazo Shule Shikizi nne (4).
*Jimbo hili lina jumla ya Sekondari 27, na zote zitachukus Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza (Form I) mwakani (Jan 2023)
*Kati ya Sekondari hizi 27, Sekondari za Binafsi ni 2, na za Serikali/Kata ni 25.
Baadhi ya Kata zimeamua kujenga sekondari nyingine zaidi ili kutatua matatizo ya umbali mrefu wa wanafunzi wanaoutembea kwenda masomoni, na vilevile kutatua tatizo la msongamano wa wanafunzi madarasani. Sekondari mpya 5 zimepangwa kujengwa, na ujenzi umeanza kwa baadhi ya Kata.
MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZETU
*Ni Sekondari tatu (3) tu zenya Maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) zilizokamilika na zinatumika ipasavyo. Sekondari nyingine zinatumia vyumba vya madarasa kuwa Maabara zao zinapohitajika!
Kwa hiyo, Tsh Milioni 75 (Tshs 75m) za Mfuko wa Jimbo zilizopokelewa hivi karibuni, zitatumika kuchangia ujenzi wa Maabara hizo 3 kwenye baadhi ya Sekondari zetu.
Sekondari zinazohitaji kuchangiwa vifaa vya ujenzi vya Maabara zao, zinaelekezwa kutuma maombi yao kwa Katibu wa Kamati ya Fedha za Mfuko wa Jimbo (Afisa Mipango wa Halmashauri yetu) kabla ya tarehe 10 Januari 2023.
Usisahau kutembelea Tovuti ya Jimbo letu, ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
Ofisi ya Mbunge
JImbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumatano, 21.12.2022
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇