LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 22, 2022

RIDHIWANI KIKWETE AMPONGEZA ANNE KILANGO KUANZISHA MASHINDANO SAME

 





 Naibu Waziri wa  Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete  amempongeza Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela kwa kuanzisha Mashindano ya Kilango Cup kwani yanaleta umoja na mshikamano kwa wananchi.


Akizungumza kwenye fainali za mashindano hayo Ridhiwani Kikwete amesema mbali ya kujenga umoja na mshikamano pia yanasaidia kuibua vipaji vya soka kwa vijana wa Tanzania kuepukana na maswala ya kiuhalifu.

Aidha amesema malengo mengine ya mashindano hayo ni kutoa elimu kuhusu umuhimu wa vijana kufanya kazi kwa bidii ili kuijenga nchi hasa kwenye kilimo na biashara.

Pia amesema michezo husaidia vijana kuachana na mambo yasiyofaa katika jamii huku akisisitiza kufanya  kazi ni msingi mkubwa wa maendeleo.

Kwa  upande wake  Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo amesema kama serikali wao wataendelea kumuunga mkono Mbunge Anne Kilango kwa juhudi kubwa anazofanya kuwaunganisha wananchi kwa pamoja kwenye maswala mbali mbali ya kuijenga nchi. 

Makamu Mwenyekiti Ccm Taifa mstaafu, John Malecela amesema anatoa shukrani za dhati kwa viongozi na Wananchi wote waliojitokeza kuangalia michuano hiyo ambayo timu zaidI ya 36 zimeungana na kushiriki mchezo wa mpira wa miguu. 

Amewasihi wananchi kulinda amani ya nchi na mshikamano kwa pamoja hili kuleta maendeleo na kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kwa wananchi wake kuleta maendeleo. 

Pia aliwaomba vijana kwa ujumla kulinda amani ya nchi na kuwa wazalendo na kuendeleza amani ya nchi kwani michezo pia ni amani na mshikamo wa watu kwa pamoja 

 Pia Mbunge wa Same Mashariki Anne kilango amesema mashindano haya ni endelevu na lengo ni kuwaweka vijana wawe pamoja na kutengeneza mshikamano na mahusiano mazuri kwenye kuleta maendeleo

Pia amesema zaidi ya vijana 1200 wameshiriki mashindano hayo na kusisitiza kuwa mashindano hayo ni juhudi za kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwani na yeye ni mmoja wa wadau wanaopenda michezo hapa nchini .

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages