LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 3, 2022

WAZIRI NDUMBARO: HESHIMA YA MAWAKILI WA SERIKALI HAIWEZI KUSHUKA KAMA MANA, LAZIMA IJENGWE

Na Mwandishi Maalum, DODOMA
Waziri wa Katibana Sheria  Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema, heshima na hadhi ya mawakili wa Serikali nchini haiwezi kushuka kama mana, bali ni kwa uongozi wa Chama cha Mawakili wa Serikali (PBA) kuhakikisha heshima na hadhi hiyo vinajengwa.

Ameyasema hayo leo Novemba 3, 2022,  wakati ujumbe wa viongozi wa PBA ukiongozwa na Rais wa Chama hicho Wakili Msomi Michael Marcellus Luena ulipofika Ofisini kwake mtaa wa Mtumba, Jijini Dodoma kujitambulisha.

Chama cha Mawakili wa Serikali kilizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali uliofanyika Septemba 29, 2022, Jijini Dodoma na baada ya Mhe. Rais kuzindua chama hicho, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt. Eliezer Feleshi kwa mamlaka aliyonayo aliteua viongozi wa mpito.

Viongozi walioteuliwa ni Wakili Msomi Michael Marcellus Luena ambayeniRais,  MakamuRaisniWakili Msomi Lucas Charles Malunde,  MwenyekitiniWakili Msomi Stephano SebaMbutu, Makamu Mwenyekiti Wakili Msomi Hassan Mayunga, Katibu akiwa ni Wakili Msomi Sia Beatrice Mrema na Muweka Hazina Wakili Msomi Irene Joseph Luselie.

“Wanachama wenu wanataka kuona wanathaminiwa na wanahadhi, na hili haliwezi kushuka kama mana, ni moja ya jukumu lenu kama viongozi pamoja na mambo mengine, kuwafanya wajisikie hivyo”, akasema Waziri  Ndumbalo.

Katika mazungumzo hayo ambayo yalihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Mary Makondo, Waziri Ndumbaro amebainisha kuwa katika nchi nyingine, Wakili wa Serikali au  Mwanasheria wa Serikali anaheshimika sana na ana hadhi ya juu.

“Kwa hiyo, mna kazi kubwa ya kufanya 'branding' ya chama chenu lakini pia ya Mawakili wa Serikali, Chama lazima kionekane kipo na kinafanyakazi.” akasisitiza Waziri Ndumbaro.

Akielezea zaidi kuhusu kusafisha taswira ya Mawakili wa Serikali, Waziri wa Katiba na Sheria alitoa mfano akisema; “Jana (Jumatano), kulikuwa na mjadala mkali Bungeni kuhusu mikataba, mpaka ikaonekana Wanasheria ni wa hovyo, lakini wakati mwingine shida si wanasheria kwa hiyo mnayo kazi ya kusafisha taswira ya wanasheria wa Serikali”.

Ameutaka uongozi huo kuhakikisha, Mawakili wa Serikali popote walipo kutoruhusu mkataba wowote kutumika bila ya kupita kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali lakini pia kuhakikisha wanashirikishwa na kuhusika katika hatua zote zikiwemo za majadiliano ya mkataba husika.

Waziri Ndumbalo pia ameuagiza uongozi huo kutetea maslahi na stahiki za wanachamawao, akisema;
“Unakuta wakili wa serikali anasimama mahakamani kuitetea serikali kwenye kesi zinazohusu mabilioni ya fedha lakini hali yake kwa maana stahiki zake na maslahi yake ni suala jingine hivyo mnao wajibu pia wakulifanyia kazi hili la maslahi bora ya wanachama wenu.
 
Katika hatua nyingine Waziri Ndumbalo ameutaka uongozi huo kuwa na mahusiano ya karibu na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na pia kuwataka viongozi hao kujenga mazingira mazuri yatakayokiwezesha Chama cha Mawakili wa Serikali kushiriki na kutoa mchango wao katika mijadala mbalimbali inayohusu masuala ya Sheria zikiwemo sheria zinazopelekwa Bungeni.

Awali Rais wa PBA Wakili Msomi Michael Luena akielezea nia ya ziara hiyo, alisema pamoja na kujitambulisha lakini pia wajumbe wameanza vikao vyao vya awali vya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Chama hicho.

Viongozi hao wameahidi kuyafanyiakazi masuala yaliyoainishwa na  Waziri Ndumbaro kwa mstakabali wa chama na wanachma wao.

Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro akiwa na Viongozi wa Chama cha Mawakili wa Serikali (PBA) Viongozi hao walipomtembelea Ofisini kwake Mtumba Jijini Dododma na kuwa  na Mazungumzo  naye, leo. (Picha na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages