LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 2, 2022

RAIS SAMIA AENDA CHINA LEO NA KUWA KIONGOZI WA KWANZA AFRIKA TANGU RAIS XI ACHAGULIWE HIVI KARIBUNI KUWA KATIBU MKUU WA CPC NA TANGU MLIPUKO WA UVIKO-19 MWAKA 2019

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Rais wa Tanzana Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuondoka leo Jumatano, Novemba 2, 2022, kwenda China kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Xi Jinping, ikiwa ni ziara ya kwanza kufanywa na Kiongozi wa juu kutoka Bara la Afrika tangu Rais Xi achaguliwe na Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa muhula wa tatu.

Taarifa iliyotolewa jana usiku na Ikulu, Jijini Dar es Salaam, imesema Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ziara hiyo ya kikazi ambayo inaaza leo Novemba 2 hadi 4, 2022, vilevile itakuwa miongoni mwa ziara za mwanzo za viongozi wa Kitaifa kutembeea China tangu utokee mlipuko wa UVIKO-19 mwezi Desemba 2019.

Taarifa imesema, Rais Samia atapokelewa rasmi kesho Novemba 3 katika ukumbi wa Great Hall Of the People ambako atafanya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais Xi na kushuhudia utiaji saini wa mikataba mbalimbali.

Mbali na kukutana na Rais Xi, Rais Samia anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Li Kengang na Spika wa Bunge la China Li Zhanshu.

"Ziara ya Rais samia inafanyika katika kipindi ambacho Tanzania na China zimeadhimisha miaka 58 ya mahusiano ya kidiplomasia. Viongozi hao wawili wanatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano katika nyanja za siasa, uchmi, utamaduni na uhirikiano wa Kimataifa", imehitisha taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages