LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 11, 2022

BALOZI WA TANZANIA MSUMBIJI BALOZI KASIKE AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA MFALME MSWATI WA ESWATINI

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji Balozi Phaustine Kasike, akiwasillsha Hati za Utambulisho kwa Mfalme Mswati wa Eswatini, jana Novemba 10, 2022

Pamoja na kuwasilisha Hati zake za Utambulisho, Balozi Kasike pia alipata fursa ya kukutana na Viongozi mbalimbali wa nchi hiyo akiwemo, Waziri wa Biashara na Viwanda ambaye pia anakaimu nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje. Aidha, alikutana na Wanadiaspora wa Tanzania waishio Eswatini.

Mbali na Msumbiji, Balozi Kasike pia anaiwakilisha Tanzania katika Jamhuri ya Madagascar na Ufalme wa Eswatini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages