LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 11, 2022

WAFU, MAJERUHI WA AJALI YA PRECISION AIR BUKOBA KULIPWA MABILIONI

Kamishna wa Bima wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA),Dkt Baghayo Saqware amesema kuwa kampuni za bima za ndani na nje ya nchi ambazo zilikatwa na Kampuni ya Ndege ya Precision Air, zitawajibika kuwalipa fidia waathirika wa ajali ya ndege hiyo yaani ndugu wa marehemu na walionusurika. Amebainisha hayo wakati wa semina na wabunge kuhusu usalama barabarani iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa jijini Dodoma Novemba 10, 2022. Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Vita Kawawa ameitaka TIRA kuhakikisha waathirika hao wanalipwa haraka fidia hiyo.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Dkt Saqware  akielezea ulipwaji wa fidia hiyo....

/>

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages