Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia
ni daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu Prof. Wiliam Mahalu
akiongoza kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam.
Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge akitoa taarifa ya utendaji
wa kazi zilizofanywa na taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi
Septemba 2022 katika mwaka wa fedha wa 2022/23 wakati wa kikao cha kwanza cha
Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Prof. Wiliam Mahalu wakati wa kikao cha kwanza cha bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye ni Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Adrea
Pembe akichangia mada katika kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi
karibuni jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mjumbe wa Bodi hiyo ambaye ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Mohamed Janabi.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA.Godfrey
Kilenga kutoka ofisi ya Managing Partner TAB Consultant Audit Firm in Tanzania akichangia
mada katika kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi hiyo Harun Matagane kutoka ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇