LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 24, 2022

SUBIRA MGALU ATOA NENO KUHUSU RAIS SAMIA KWA WAJUMBE UWT BAGAMOYO

Na Scola Msewe, Bagamoyo

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Mgalu, amewaambia Wajumbe 645 wa Mkutano Mkuu wa UWT Wilaya ya Bagamoyo mkoani hapa kwamba, wakawe wajumbe wa kuyasemea mazuri yanayotekelezwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu CCM iendelee kupata ushindi wa kishindo.


Amesema hayo wakati alipopewa nafasi ya kuzungumza katika Mkutano Mkuu wa UWT Wilaya ya Bagamoyo kwaniaba ya Wabunge wa Mkoa wa Pwani iliyofanyika Lugoba Chalinze uliokuwa chini ya Usimamizi wa Mkuu wa Wilaya hiyo Zainab Issa Abdallah.


Subira amesema akinama wa UWT kuanzia ngazi ya mashina, matawi na kata ndio jeshi la ushindi wa CCM hivyo kila mwanamke katika nafasi yake akakinadi CCM katika ngazi yake na Kijiji na mtaa wake ili CCM iendelee kushika hatamu sambamba na Kuhakikisha Rais Samia anapata kura za kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.


Amesema Uchaguzi mkuu wa UWT Wilaya ni miongoni mwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa taifa ujao ambao kwa Mara kwanza nchini yetu itasimamisha Mgombea Urais mwanamke ambaye Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Akinamama wa UWT ndio wa kwenda kumsemea kwa Wananchi kila Kona.


Subira ameyataja baadhi yaliyofanyika nchini ambayo yanawapa raha na ujasili wa kutembea kifua wanawake kuwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa 15000 na kusababisha wanafunzi wote waliofaulu darasa la Saba kuingia kwa wakati mmoja kidato cha kwanza.


Mengine ni pamoja na ukamilishaji wa maboma ya Zahanati 61 na ujenzi wa vituo vya afya kumi vya kutokana na fedha za tozo na kufanya tarafa zote za mkoa wa Pwani kuwa na vituo vya afya huduma za afya za uhakika ni kila tarafa na hata Sasa huduma za upasuaji kufanyika katika kituo cha afya Msoga.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages