LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 24, 2022

HAWA NDIO VIONGOZI WAPYA UVCCM WILAYA KIBAHA MJINI, KAZEMBE ASHIKA USUKANI

Na Dismas Lyassa, Pwani

HATIMAYE vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wamekamilisha uchaguzi katika Wilaya ya Kibaha Mjini, Pwani kwa kumchagua Ramadhan Kazembe kuwa mwenyekiti wao na nafasi kujaza  nyingine zote za uongozi katika jumuiya hiyo.


Pichani ni mwenyekiti mpya UVCCM Wilaya Kibaha Mjini Ramadhan Kazembe (kushoto) akiwa na Katibu wa jumuiya hiyo UVCCM Kibaha Mjini, Amina Makona.

Akitangaza matokeo, msimamizi wa uchaguzi ambaye ni katibu wa Umoja wa Wanawake  Mkoa ,Fatuma Ndee alisema Kazembe ameshinda kwa kupata kura 177, akifuatiwa na 
Godlove Rwekaza aliyekuwa akitetea nasfasi hiyo kura 84 na Nancy Matta 55 .

Katibu wa UVCCM Kibaha Mjini, Amina Makona alishukuru kwa mchakato kufanyika kwa utulivu tangu hatua za awali za uchukuaji fomu hadi kutangazwa matokeo. 

                                      MAPOZI TOFAUTI YA WAJUMBE! 

            Pichani juu ni wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi

Makona aliwataka kujituma, kuwa wabunifu na utumishi uliotukuka. Kwa wale ambao kura hazijatosha, wameshauriwa kutokata tamaa akisema kumalizika kwa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine.

MATOKEO ZAIDI

1. MJUMBE WA H/KUU MSHINDI  NI:-
NDG. JONAS REMMY NGWESA

2. MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA MSHINDI NI:-
NDG. VALENTINE MBAWALA

3. MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM WILAYA MSHINDI NI:-
NDG.HAPPINESS EUSTACE

4. WAJUMBE WA BARAZA MKOA WASHINDI NI:-
NDG. NANCY MATTA
NDG. VALENTINE MBAWALA

5. WAJUMBE WA BARAZA LA VIJANA WILAYA WASHINDI NI:-
NDG. ALLY GOMBATI
NDG. BENJAMIN MJATA
NDG. ASHURA THOMAS
NDG. MWASITI NZOTA
NDG. ABUU MATUMLA

6. WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA VIJANA MKOA WASHINDI NI:-
NDG. SABRA SAID
NDG. WILLIAM MJATA
NDG. ABUU MATUMLA

7.UWAKILISHI U.W.T MSHINDI NI:-
NDG. MARIA MSIMBE

8.UWAKILISHI WAZAZI MSHINDI NI:-
NDG. HAMISI KASHORO

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages