Na Jastin Cosmas, Kigoma
Halmashauri kuu ya chamama cha mapinduzi CCM mkoa wa Kigoma katika kikao chake kilicho kutana tarehe 21 septemba 2022 chini ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kigoma Amandusi Nzamba pamoja na mambo mengine imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Sulihu Hassan kwa hatua mbalimbali anazo zichukua katika kuanzisha kuendeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Taifa.
Halmashauri kuu imetoa pongezi hizi baada ya kuridhishwa na kasi ya kiwango cha juu iliyo wezesha mkoa wa kigoma kuanza kuunganishwa katika gridi ya Taifa ya umeme jambo ambalo lilitarajiwa kufanyika mwaka 2023 mkoa wa kigoma umeanza kuunganishwa katika gridi ya Taifa tarehe 17/9/2022 kwa wilaya za Kakonko na Kibondo ambapo kesho tarehe 22/9/2022 ifikapo saa 12 jioni wilaya Kasulu zitakuwa zimeunganishwa katika gridi ya Taifa.
Aidha kwa mjibu wa maelekezo ya serikali yaliyo tolewa na waziri wa nishati Mhe.January Yusufu Makamba ndani ya siku 30 kutoka leo tarehe 22/9/2022 wilaya ya Kigoma na Uvinza pia zitakuwa zimeunganishwa na gridi ya Taifa na hivyo kufanya mkoa mzima wa Kigoma kutumia umeme wa gridi ya Taifa.
Chama cha mapinduzi CCM katika mkoa wa Kigoma, wawakilishi wa wananchi (wabunge, Madiwani) pamoja na wananchi wote wa mkoa wa Kigoma tuna mpongeza na kumshukuru Rais wetu kwa heshima kubwa ya kutufuta machozi ya muda mrefu ya kukosa umeme tosherezi kwa shughuli za maendeleo tokea nchi yetu ipate uhuru mwaka 1961.
Pamoja na rais tunawapongeza wote wanao msaidia akiwemo makamu wa Rais Philip Mpango waziri mkuu na mlezi wa mkoa wetu Mhe M. Majaliwa waziri mwenye dhamana ya nishati Mhe January Makamba na uongozi wa shirika la Umeme Tanzania.
Ikumbukwe kuwa kuzimwa kwa genereta zote katika mkoa wa Kigoma na kuunganishwa kwenye gridi ya Taifa mbali na kutachochea uchumi na uanzishwaji wa viwanda lakini pia kutafanya serikali iokoe kiasi cha shilingi Bilioni hamusini na pointi sitini na mbili zilizo kuwa zikitumika kila mwaka kununua mafuta na utunzaji wa jenereta zilizopo hapa mkoani Kigoma.
Halmashauri kuu ya mkoa pia imempongeza Rais na Serikari yake kwa usikivu na huruma walio ionyesha kwa watanzania kwa kuwapunguzia na kufuta baadhi ya tozo kwenye miamara ya fedha zinazo tumwa kwa njia yasimu na benki ili kuleta unafuu kwa wananchi ni jambo la kiungwana kwa serikali iliyo chaguliwa na wananchi kufanya juhudi za kupata fedha kwa ajili ya maendeleo pia kufanya tathimini kila wakati ili michango ya wananchi kwa taifa lao isiwaachie madonda katika maisha yao ya kila siku
Mhe Rais wetu usikivu na huruma yako kwa wananchi wako ni nguzo mhimu katika kujenga umoja wa kitaifa endelea hivyo na sisi tupo pamoja nawe kiongozi wetu tunakuombea afya njema na maisha marefu yenye hekima na busara katika kuliongoza Taifa letu.
Kwa upande wake katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa kigoma Feruzi .M.Feruzi amesema kuwa chama cha mapinduzi mkoa wa Kigoma kimeimalisha mahusiano mazuri na nchi zinazopakana na mkoa wa Kigoma nchi hizo ni pamoja Burundi Kongo na Zambia ambapo umeme huo wa gridi ya Taifa utaleta tija kwa kuanzisha viwanda pamoja na kupanua wingo wa kibiashara.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇