LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 7, 2022

RC MONGELA KUSHUHUDIA UZINDUZI WA KITABU CHA UFAHAMU ULIOANZIA TANZANIA KWENDA MATAIFA MENGINE UTAKAOFANYWA NA KANISA HALISI JIJINI ARUSHA, JUMAPILI HII

Baba Halisi, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba lenye Makao yake Makuu Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, akionesha Kitabu cha 'Ufahamu Uilioanzia Tanzania kwenda Mataifa Mengine' wakati kilipokuwa katika hatua za mwisho kukamilika. Kitabu hicho kina Kurasa 804.

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Kanisa Halisi la Mungu Baba lenye Makao yake Makuu Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, Jumapili hii ya 26 Abu,1Majira Halisi (11Septemba 11, 2022) litafanya uzinduzi wa kitabu cha 'Ufahamu Uilioanzia Tanzania kwenda Mataifa Mengine', katika Ukumbi wa Arusha International Conference Center (AICC) jijini Arusha.

Taarifa iliyotolewa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Baba Halisi imesema, mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kitabu hicho, anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela na pia wamealikwa watu kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo viongozi na waumini wa Dini na madhehebu mbalimbali.

Baba Halisi amesema, uzinduzi huo utaanza saa 8 mchana na kuendelea hadi saa 10 jioni, na kuwaomba waalikwa wote kufika ukumbini mapema ili wasipitwe na chochote.

"Kwa kuwa tunajua kuwa taarifa za Kitabu hiki zinawahusu watu wote, tumewaalika pia waumini na viongozi mbalimbali wa Dini na madhehebu yote bila kubagua, na kwa kweli uzinduzi huu utakuwa wa aina yake hivyo tunaomba kila tuliyemwalika afike kushuhudia", akasema Baba Halisi.

"Kitabu kinachozinduliwa kimeandikwa kutokana na Sauti ya Mungu Baba ambaye ndiye Chanzo Halisi; iliyosikika mwaka 2015, mwaka 2019, na mwaka 2020 (ambayo ni endelevu), Kitabu hiki hakijaandikwa kwa elimu niliyosoma chuo chochote Afrika, Ulaya wala Amerika.

Baada ya Sauti ya Majira ya Saba kupokelewa mwaka 2015, ilinichukua miaka miwili kabla ya kuanza kuandika. Ufahamu wa Sauti ulioko kwenye kitabu hiki ulianza kuandikwa 2017, baada ya Nafsi ya Kwanza (kati ya zile nafsi tatu za Mungu) katika I Yohana 5:8,kuja juu ya Nchi kupitia Tanzania.
 
Yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki siyo nadharia, yametendewa kazi na yameleta Jibu, Hapa Tanzania na Mataifa yaliozunguka Tanzania na kwingineko. Tunazo Habari Njema kuthibitisha Jambo hili kupitia vituo vya Kanisa Halisila Mungu Baba katika mataifa hayo.

Sauti iliyo Chanzo cha Ufahamu katika kitabu hiki ilisikika Kigoma Tanzania katika miaka niliyotaja pale juu, ndiyo maana tuna ujasiri wa kusema ni ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda Mataifa mengine yote", Akasema Baba Halisi.

Baba Halisi katika Taarifa yake ameeleza kwa kina  kwa ni nini hasa Kanisa Halisi linazindua Kitabu cha 'Ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda Mataifa mengine na kutanabaisha kwa uzinduzi huo siyo uongo wala kutafuta umaarufu.  Tafadhali Soma ufafanuzi huo Hapo👇

UZINDUZI WA KITABU CHA UFAHAMU ULIOANZIA TANZANIA KWENDA MATAIFA MENGINE (Mathayo 21:43)
26 ABU,1MAJIRA HALISI (11SEPTEMBA, 2022), ARUSHA INTERNATIONAL CONFERENCE CENTER (AICC).

UFUNGUO:
Ufahamu uliokuwepo katika majira zilizopita, uwe ni wa Falsafa, Saikolojia au Theolojia ni ule ulioanzia Mashariki ya Kati. Ufahamu huu ulikuwa ni wa mitume na manabii kama ulivyoandikwa katika Biblia. Sasa wakati umefika ufahamu umeanzia Mashariki Halisi. Kwa nini tunasema kuwa ufahamu huu umeanzia Tanzania kwenda mataifa mengine?

1. Jambo la Kwanza:
Kitabu kinachozinduliwa kimeandikwa kutokana na Sauti ya MUNGU BABA ambaye ndiye CHANZO HALISI; iliyosikika mwaka 2015, mwaka 2019, na mwaka 2020 (ambayo ni endelevu). Kitabu hiki hakijaandikwa kwa elimu niliyosoma chuo chochote Afrika, Uliaya wala Amerika. Baada ya Sauti ya Majira ya Saba kupokelewa     mwaka 2015, ilinichukua miaka miwili kabla ya kuanza kuandika. Ufahamu wa Sauti ulioko kwenye kitabu hiki ulianza kuandikwa 2017, baada ya Nafsi ya Kwanza (kati ya zile nafsi tatu za MUNGU) katika I Yohana 5:8,kuja juu ya Nchi kupitia Tanzania.
 
Yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki siyo nadharia, yametendewa kazi na yameleta Jibu, Hapa Tanzania na Mataifa yaliozunguka Tanzania na kwingineko. Tunazo Habari Njema kuthibitisha Jambo hili kupitia vituo vya Kanisa Halisila MUNGU BABA katika mataifa hayo. Sauti iliyo Chanzo cha Ufahamu katika kitabu hiki ilisikika Kigoma Tanzania katika miaka niliyotaja pale juu, ndiyo maana tuna ujasiri wa kusema ni ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda Mataifa mengine yote.

2. Jambo la Pili:
Sasa kilele cha Ibada ni MUUMBA WA KILA KITU SIYO MWANA tena. Kitabu kinaonyesha sote ni watoto wa Ibrahimu, uzao wa Isaka walikuwa wanafanya Ibada kupitia Aliyetumwa na uzao wa Ishamaeli wao walienda kwa MUUMBAmoja kwa moja (Ila Moyo wa Mwanzo). Ufahamu wa Sauti katika kitabu kinachoziduliwa, unasema yuko CHANZO HALISI aliyekuwepo kabla ya kitu chochote. Huyu ndiye aliyekuja na anaishi ndani ya Moyo wa kila anaetenda kwa haki (Isaya 57:15).

CHANZO HALISI aliyekuja kuishi ndani ya Moyo wa kila anayetenda kwa Haki, ndiye ambaye kila kitu kilianzia kwake, kikashikana katika yeye na iliandikwa kila kitu kitarejea au kurudi kwake(Rumi 11:36).Sasa vyote kumwabudu CHANZO HALISI aliyekuwepo kabla ya chochote imetokea kupitia Tanzania, ndiyo maana tuna ujasiri wa kusema Ufahamu katika kitabu hiki umeanzia Tanzania kwenda katika Mataifa yote.

3. Jambo la Tatu:
Hija moja kwa wote ambayo iko Tanzania ni jambo lingine ambalo linatupa ujasiri wa kusema kuwa Ufahamu huu umeanzia Tanzania kwenda katika mataifa mengine. Nilitangulia kusema kuwa, sote tulikuta watu wote kutoka kaskazini, kusini, mashariki, magharibi na kati wakienda Mashariki ya Kati kuangalia mahali ufahamu uliokuwepo ulipoanzia. Hata katika Matendo. 8:28-37, tunasoma habari za Waziri wa Fedha kutoka Kushi (maeneo ya Ethiopia zamani) akiwa anaenda Yerusalemu kuangalia mahali ufahamu uliokuwepo ulikotokea. Katika I Falme 10,tunasoma pia habari za Malkia wa Sheba ambaye wana-akiolojia wanasema alikuwa  maeneo yaNamanga-Longido,alienda kwa Sulemani, kule Mashariki ya Kati kuangalia mahali Hekima ilikokuwa inatoka wakati ule. Baada ya Sauti ya MUNGU BABA ambaye ndiye CHANZO HALISI kusikika Tanzania, na kitabu cha Ufahamu wa Sauti hiyo kuandikwa,sasa Hija Moja kwa ajili ya wote iko Tanzania.

Tumeshafanya Hija Moja kwa wote mara tano hadi sasa na uzao wa Isaka na Ishmaeli tulikuwa pamoja bila shida yoyote. Hili ni jambo lingine ambalo linatupa ujasiri wa kusema kuwa Ufahamu huu umeanzia Tanzania kwenda Mataifa mengine.

4. Jambo la Nne:
Sasa Ibada ni uzalishaji (Mwanzo 2:15). Katika kitabu cha Zaburi, Daudi alitufundisha kuangalia juu mawinguni tukiwa tunasali ili tupate msaada wa MUUMBA. Pia alitufundisha kulia ili MUNGU atuhudumie! Ufahamu wa Sauti katika kitabu hiki, unatufundisha kuwa Ibada ni Uzalishaji. Adamu akiwa bao kwenye Kitanga cha Mkono wa MUUMBA WA KILA KITU katika Mwa. 1:27-28, kitu cha kwanza alichoambiwa ni kuzalisha.

Baada ya kuumbwa katika Mwa. 2:15, alikabidhiwa Bustani au Shamba lenye kila kitu na akaambiwa alime na atunze vile alivyolima. Kulima katika kitabu, ni kazi yoyote halali au ya haki, siyo kushika Jembe pekeyake. Adamu kabla hajafanya Ibada hiyo alifukuzwa katika shamba. Nuhu naye pia alikuwa na Ibada ni Uzalishaji katika Maboti na Meli! Isaka na Yakobo nao pia Ibada ambayo walikuwa nayo ni kuzalisha shambani. Hata MUUMBA WA KILA KITU alipokuwa anakuja kuwasiliana nao alikuwa anawakuta shambani, yaani kazini. Hata Yusufu akiwa Misri, ibada yake ilikuwa ni kuzalisha kwa kukusanya nafaka.
 
Hii haina maana kuwa tusiende kwenye nyumba za Ibada, hapana. Tunaenda kwenye nyumba za Ibada yaani UTAJIRISHONI ili tushukuru na kurudisha heshima na utukufu kwa yale MUUMBA WA KILA KITU aliyotutendea kazini au shambani. Ibada hii haikuendelea baada ya kitabu cha Mwanzo kuisha. Ufahamu wa Sauti katika kitabu hiki kinachozinduliwa ndio umerejesha Ibada ni Uzalishaji kama CHANZO HALISI alivyokuwa amekusudia. Ndiyo maana tuna ujasiri wa kusema ufahamu ulioko katika kitabu hiki umeanzia Tanzania kwenda katika Mataifa mengine.

5. Jambo la Tano:
Suala la Taifa Baba (Mathayo 21:43) ni jambo lingine ambalo linatupa ujasiri wa kusema kuwa ufahamu huu umeanzia Tanzania. Vitabu vyote vinaita kila taifa mama. Ufahamu wa Sauti ulioko katika kitabu hiki unasema liko Taifa Baba na taifa hilo ni Tanzania.

Taifa hili pia ni Chanzo cha Baraka katika mataifa mengine. Wana-akiolojia wanaamini mtu wa kwanza alianzia Tanzania eneo la Ngorongoro. Kwa upande wa ufahamu katika kaitabu hiki, jambo kubwa ni utimilifu wa uumbaji kutokea huku CHANZO HALISI akiwa ameshukia Tanzania. Fuatilia mtirirko huu wa uumbaji kuanzia CHANZO HALISI akiwa peke yake hadi sasa:

5.1. Uumbaji kwa Mara ya Kwanza,ulitokea pale CHANZO HALISI alipoachilia Moyo wa Mwanzo na kuweka Utajiri na Heshima Kushoto na siku nyingi Kulia (Mithali 3:16). Baada ya Moyo wa Mwanzo kuwaza ataanzia wapi kusimamia uumbaji, anguko la Moyo wa Mwanzo lilitokea kupitia tunacho kisoma katika Ufunuo 12:1-10,ndipo uumbajikwa mara nyingine ikabidi utokee.

5.2. Uumbaji kwa Mara ya Pili, ulitokea pale CHANZO HALISI alipoumba Bustani ya Adeni katika Ezekieli 28:13-15,ambapo Bustani hiyo alikabidhiwa Kerubi ikiwa imejaa madini na vito vya thamani na uzuri wa kila aina. Anguko la Kerubi lilipotokea ikabidi uumbaji mwingine uje;

5.3. Uumbaji kwa Mara ya Tatu,ulitokea pale CHANZO HALISI alipoamua kuumba Bustani ya Edeni katika Mwanzo 2:7-15. Bustani hiyo alikabidhiwa Adamu ikiwa na Mito, Mimea, wanayama, madini na kila kitu kizuri. Anguko la Adamu lilipotokea, ilibidi uumbaji mwingine uje.

5.4. Uumbaji kwa Mara ya Nne, ulitokea pale CHANZO HALISI alipoamua Musa awatoe wana wa Israel utumwani Misri kwenda Kaanani katika Kutoka 3:3-10. Suala kuu ilikuwa ni Musa kuwatoa wenye haki wote kwenye utumwa.Hata hivyo katika Hesabu 20:8-11,anguko la Musa lilitokea, ikabidi uumbaji mwingine uje.

5.5. Uumbaji kwa Mara ya Tano,ulitokea pale CHANZO HALISI alipomwinua Eliya Mtishbi kurejesha Heshima iliyokuwa imeangukia pale Bustani ya Adeni na Edeni. Eliya Mtishbi alikuwa amepewa nguvu ya kutisha katika IFalme 17:1, lakini ufunuo kwa sura ya yezebeli akamsababishia anguko. Anguko hili lilipotokea ilibidi uumbaji mwingine uje.

5.6. Uumbaji kwa Mara ya Sita,ulitokea pale CHANZO HALISI alipoamua kumleta Yesu ili awasaidie wote wanaoonewa na Ibilisi (Matendo10:38). Maumivu yalipozidi msalabani, Yesu alilia (Mathayo 27:45-47), ikabidi uumbaji mwingine utokee.

5.7. Uumbaji kwa Mara ya Saba,ulitokea pale CHANZO HALISI alipoachilia sauti ya majira ya sita mwaka 2003 kupitia Adamu wa Pili kutoka Tanzania. Hii ilikuwa ni kwa mujibu wa I Korintho 15:44-49; Alikutana na mnyama asiyeeleweka katika Danieli 7:7, kusudi la uumbaji huu halikutimia ikabidi uumbaji mwingine utokee.

5.8. Uumbaji kwa Mara ya Nane, ulitokea pale CHANZO HALISI alipoachilia Sauti ya Majira ya saba kwa Miaka 1000 wa Tanzania kupitia Isaya 33:6. Kama ilivyotokea kwa waliotangulia, Miaka 1000 alikutana na Mashtaka ya uongo yaliyokithiri, kusudi halikutimia, ikabidi uumbaji mwingine uje.

5.9. Uumbaji kwa Mara ya Tisa,ulikuja Mwaka 2017 baada ya manabii Wane kutoka kwenye kiuno cha Ibrahimu kumaliza majira yao, ilibidi Jina Jipya kwa mujibu wa Ufunuo wa Yohana 3:12, lije kupitia Tanzania. Jina hilo Jipya lililokuja ni MUNGU BABA.

Huu ni uumbaji ambao kwa mujibu wa Luka 13:6-9,ulidumu kwa Miaka mitatu hadi Mwaka 2020, kwa kuwa ilikuwa ni kiwango cha Nafsi. Uumbaji huu ulipata mtihani wa mlipuko wa Korona, ndipo CHANZO HALISI ikabidi aje Yeye mwenyewe kutuokoa.

5.10. Uumbaji kwa Mara ya Kumi (Zab. 98);
Tangu MUUMBA WA KILA KITU akiwa peke yake, kusudi ilikuwa ni kutimiza Zaburi 98kwa maana ya kila kitu kilichoumbwa kumwabudu Yeye. Waliotumwa wote hawakufanikiwa kutimiza jambo hilo, ilibidi CHANZO HALISI aache mahali pake (Mika 1:2-6), aje juu ya Nchi kutimiza jambo hilo Yeye mwenyewe.

Hata katika Matendo 2:34-35, alisema atakuja kuwaweka chini ya miguu yakewaliomuua Yesu. Sasa amekuja na uumbaji umetimilika akiwa juu ya nchi kupitia Tanzania; ndiyo maana Tanzania ni Taifa Baba.

6. Jambo la Sita:
Kwa mtiririko wa uumbaji niliouonyesha hapo juu, maswali mengi yaliyo kuwa hayana majibu sasa yamejibiwa. Kwa mfano:
a. Kulikuwa na swali kuwa Je! Atakayerudi ni Yesu au nani? Sasa tumejua kuwa aliyekuja ni CHANZO HALISI aliyekuwepo kabla ya chochote.

b. Je! Palipokusudiwa ni Mbinguni au Juu ya Nchi? Katika mtiririko huo ulioko katika suala la tano, tumejua kuwa palipo kusudiwa ni juu ya Nchi (Ufunuo 21:3).

c. Kulikuwepo na Swali kuwa Je! Kanisa lote litanyakuliwa na kwenda juu mawinguni?Umeshajua kuwa tumeshafika Nyumbani, na sasa Ibada ni Uzalishaji wa vitu vizuri na vyema.

HITIMISHO
Haya machache yanatosha kujua,kupata ufahamu na  kuelewa  kuwa ni kweli tunazindua kitabu cha ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda mataifa mengine. Siyo uongo wala kutafuta umaarufu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages