Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela jana amezindua Kitabu cha 'Ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda Mataifa Mengine' katika hafla ya kufana iliyofanyika katika ukumbi wa Arusha International Conference Center (AICC) jijini Arusha, na kusema kitabu hicho ni baraka na tunu ya Taifa la Tanzania.
Baada ya RC Mongela kuzindua Kitabu hicho, Baba Halisi ambaye ni Kiongozi Mkuu Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba lenye Makao yake Makuu Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, alimkabidhi nakala ampelekee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
"Kitabu hiki nimekisoma, japo siyo chote maana nikikubwa sana, lakini kwa sehemu niliyosoma, nimeona Baba Halisi uliyoandika humu ni maono makubwa siyo kwa binadamu tu bali kwa Taifa la Tanzania, hivyo kitabu hiki ni tunu ya taifa na kinastahili kusomwa na kila mtu", akasema RC Mongela.
Hiki kitabu ni miongoni mwa mambo makubwa ambayo binafsi nimeyashuhudia Kanisa Halisi la Mungu Baba yakifanyika kupitia maono yako wewe Baba Halisi, hasa upande wa Utalii. Hapa Arusha Utalii ulikuwa umedorora kutokana na mambo mengi ikiwemo janga la Corona, ukaja hapa Arusha kufanya maombi maalum ya kuinua utalii.
Naamini hiki kinachofanywa na Kanisa Halisi, mfano ni baada ya maombi yale, katika hali ambayo hakuna aliyetarajia, Rais Samia Suluhu Hassan akaja na wazo la kukuza Utalii kupitia filamu ya 'Royal Tour' ambayo kwa kweli imeleta ufanisi mkubwa katika sekta ya utalii", akasema RC Mongela.
"Kwa sasa utalii Arusha umekua, Watalii wamekuwa wengi na kama mnavyojua utalii ukikua vipato vinaoonezeka kwa wanaojishughulisha na sekta hii na wadau wote, kwa hiyo hili pia limeendana na dhana ya 'Ibada ni Uzalishaji inahubiriwa na Kanisa Halisi la Mungu Baba", akasema RC Mongela.
Alilipongeza Kanisa Halisi kwa Mahubiri yao ya kusisitiza katika mambo matatu ambayo ni Amani, Upendo Usio bagua na Uzalishaji, akisema mambo hayo ni muhimu sana kwa sababu ndiyo ambayo hata Rais Samia amekuwa akisisitiza kila siku kufanyika hapa nchini.
"Mnaposema Amani, upendo usiobagua na Ibada ni uzalishaji, japo mambo haya mnayasema kiimani, lakini kwa kweli ndiyo ambayo hata nchi na dunia kwa jumla inayahitaji, maana Rais wetu kila wakati husisitiza amani, husisitiza Watanzania kupendana lakini husisitiza zaidi kila mtu kujikita katika kufanya kazi ili kuzalisha kwa ajili ya kukuza uchumi wa kila mtu na taifa kwa jumla", akasema Mongela.
Baada ya kuzindua kitabu hicho chenya kurasa 804 na kolam mbili kila ukurasa, RC Mongela alinunua nakala mbili za kitabu hicho kwa Sh. milioni 2, na kisha kuungwa mkono na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha Zelothe Steven na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ambao nao walinunua nakala ya kitabu hicho kwa Sh. milioni moja kila mmoja.
"Mimi nimenunua kitabu hiki kwa sh. milioni 2. Lakini sasa kwa kuwa mimi ni muuza duka la CCM na mwenye duka mwenyewe Mwenyekiti wa CCM mkoa huu Ndugu Zelothe yupo hapa, hebu tumsikilize naye anasemaje", akasema RC Mongela kabla ya kumpa nafasi Zelothe kusema lolote kuhusu kitabu hicho.
Baada ya kuepwa nafasi, Mwenyekiti Zelethe alisifu kazi iliyofanywa na Baba Halisi, akisema, "kitabu hiki ulichokiandika ni alama ya kudumu ambayo hata ukiondoka duniani itabaki", kisha akaahidi kukinunua kwa sh. milioni mbili.
Akizungumza wakati akimkaribisha RC Mongela kuzindua kitabu hicho, Baba Halisi alisema, ni kitabu ambacho imemchukua miaka mitano kukiandika, na amekiandika kutokana na 'sauti' yaani ujumbe kutoka kwa Mungu Baba na siyo mambo ambayo ameandika kutokana na elimu yake ya ndani na nje ya Tanzania.
Baba Halisi alifafanua kwa kina kwa nini aliweza kuandika kitabu hicho na kueleza mengi yaliyomo ikiwemo kuhusu kwa nini Ufahamu umeanzia Tanzania kwenda Maifa mengine.
Hafla hiyo ilihudhuria na mamia ya makuhani na Uzao (waumini) kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo Makuhani wa nchi za nje waliohudhuria ni pamoja na wa Uganda, Kenya, Msumbiji, Congo DRC na Zambia
Habari Katika Picha👇
Mtiririko wa hafla hiyo 👇
Uzao wakiwasili ukumbi wa AICC kwenye hafla hiyo.
Uzao (waumini) na waalikwa wakiwa nye ya ukumbi wa AICC
Uzao (Waumini) wakichukua vitambulisho kuingia ukumbini.
Kuhani Uokovu Halisi wa Kituo cha Kanisa Halisi mkoani Arusha akiwakaribisha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango walipowasili kwenye hafla hiyo.
Ukumbini👇
Baba Halisi akianza kuendesha Ibada ya uzinduzi wa Kitabu hicho. "Sasa Wana Kwaya imbeni kwanza Wimbo wa Tanzania Imebarikiwa", akasema Baba Halisi.
Waimbaji wa nyimbo za kumwinua Chanzo Halisi wakiimba wimbo wa 'Tanzania imebarikiwa'.
'Mkaanga Chipsi' wa Bendi ya Nyimbo za kumwinua Chanzo Halisi akikoleza wimbo huo wa Tanzania imebarikiwa wakati ukiimbwa.
Makuhani wa Kanisa Halisi wa nchi za nje wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Makuhani wa Kanisa Halisi wa Nchi za Nje wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Baba Halisi akifanya Shukurani ya kuanza Ibada hiyo.
Muonekano ulivyokuwa ukumbini.
muonekno ulivyokuwa ukumbini.
Makuhani wa Kanisa Halisi la Mungu Baba wakiwa wamejipanga kusubiri kumlaki mgeni rasmi.
Mgeni rasmi RC Mongela akiwasili ukumbini👇
RC Mongela akimsalimia Mama Halisi baada ya kuingia ukumbini.
Baba Halisi akisema neno kumpokea RC Mongela Ukumbini.
"Mgeni wetu rasmi huyo hapo ameshawasili, tumshangile", akasema Baba Halisi.
"Kwa kweli tumesikia faraja sana wewe Mkuu wa mkoa kufika kwenye Hafla hii, Chanzo Halisi akubariki sana", akasema tena Baba Halisi akimkaribisha RC Mongela ukumbini.
RC Mongela akiteta jambo na Kuhani Moja baada ya kuketi.
Makuhani wakiwa wameketi kwa faraja kubwa ukumbini. Kushoto ni Kuhani kutoka Kenya.
Kuhani wa Uganda akiandika jambo wakati akiwa ukumbini. anayefuatia ni Kuhani wa Zambia.
Waalikwa ambao siyo Uzao (waumini) wa Kanisa Halisi la Mungu Baba nao walihudhuria hafla hiyo.
Kwaya ya nyimbo za kumukuza Chanzo Halisi wakiimba wimbo maalum.
Wakicharaza vyombo kushajihisha wimbo huo maalum.
Mpiga gita akihanikiza wimbo huo.
Baba Halisi akipepea kitambaa cheupe kufuahia wimbo huo.
Mama Halisi akifurahia wimbo huo.
RC Mongela, Kuhani Moja na Wokou Halisi wakifurahia wimbo huo.
Makuhani na Uzao wakifurahia wimbo huo.
Makuhani na Uzao wakirurahia wimbo huo.
Baba Halisi akimkaribisha RC Mongela kuzindua kitabu, baada ya kueleza dhima nzima ya kitabu hicho.
Baba Halisi akimkaribisha RC Mongela kuzungumza na kuzindia Kitabu hicho. "sasa itabidi niwe mlinzi wako hapa", akasema Baba Halisi.
"Sasa ukiwa mlinzi wangu hapa sitakuwa na amani, naomba Baba Halisi ukakae tu", akasema RC Mongela kabla ya kuanza kuzungumzia uzinduzi wa Kitabu hicho.
RC Mongela akizungumza.
Baba Halisi na Mama Halisi wakifurahia hotuba ya RC Mongela.
Waalikwa wakimsikiliza RC Mongela.
Askari Polisi aliyefika kwenye hafla hiyo akimsikiliza RC Mongela.
Makuhani na Uzao wakimsikiliza RC Mongela.
Wanamuziki wa nyimbo za kumwinua Chanzo Halisi wakimsikiliza RC Mongela.
Baba Halisi na Mama Halisi wakiwa wamesimama wakati RC Mongela akimaliza hotuba yake.
Baba Halisi akimshukuru RC Mongela baada ya kumaliza hotuba yake.
Baba Halisi akifanya Shukrani kuinua hotuba ya RC Mongela.
Kwaya ikitumbuiza kusindikiza Hotuba ya RC Mongela.
Baba Halisi akiwaalika kuzungumza Makuhani kutoka nje ya Tanzania.
Kuhani wa Msumbiji akizungumza. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Steven akimsikiliza kwa makini Kuhani huyo.
Kuhani kutoa Zambia akizungumza.
Kuhaki kutoka Kenya akizungumza.
Kuhani kutoka Congo DRC akizunguBaba Halisi akiendelea na Ibada.
Mwakilishi wa Sheikh wa mkoa wa Arusha Sheikh Banka Seifu na Kiongozi wa Bahai Arusha Msabi John wakipokea Shukrani iliyokuwa ikifanywa na Baba Halisi.
Baba Halisi akimkaribisha RC Mongela kuzindua Kitabu hicho.
Baba Halisi akimkabidhi RC Mongela kitabu cha kuzindua.
RC Mongela akizindua kitabu hicho.
"Naam ni kitabu muhimu", akasema RC Mongela baada ya kuzindua kitabu hicho.
Kisha akakionyesha kitabu hicho kilivyo.
Baba Halisi akafungua fungasho maalum la kitabu hicho ili kumkabidhi RC Mongela ampelekee nakala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassa,
"Basi nakukabidi kitabu hiki, nakuomba umfikishia Rais wetu Samia", akasema Baba Halisi.
Kisha Baba Halisi akampatia RC Mongela na yeye nakala ya hitabu hicho.
RC Mongela akamshukuru Baba Halisi kumzawadia kitabu hicho.
"Kwa kweli kitabu hiki ni tunu ya taifa la Tanzania nitakinunua kwa sh. milioni 2", akasema RC Mongela.
Kisha Baba Halisi akamkabidhi RC Mongela nakala mbili za kitabu hicho.
"Na mimi nitanunua Kitabu hiki kwa sh. Milioni Moja", akasema Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Steven.
Baba Halisi akamkabisi nakala ya kitabu hicho.
DC wa Arumeru Mhandisi Richard Ruyango naye akatangaza kununua kitabu hicho kwa sh. milioni moja.
Baba Halisi akamkabidhi nakala ya kitabu hicho DC Mhandisi Richard Ruyango.
Kisha akamzawadia nakala ya kitabu hicho Sheikh Banka Seif
"Asante sana Baba Halisi", Sheikh Banka akasema.
Kisha Baba Halisi akamzawadia nakala ya kitabu hicho Kiongozi wa Bahai.
RC Mongela akakabidhi kitabu kwa Kuhani Dk. Paul baada ya kununua kitabu hicho kwa Sh. milioni moja.
Akamkabidhi pia Kanisa (Mke) wa Dk. Paul kitabu naye kwa kukinunua kwa sh. Milioni moja.
Akaendelea kukabidhi nakala ya kitabu hicho kwa kila kuhani aliyekinunua kwa sh.milioni moja.
RC Mongela akiendelea kukabidi nakala ya kikabu hicho kwa makuhani.
Kuhani Moja akitangaza kununua Kitabu hicho kwa sh. Milioni moja.
RC Mongela akikabidhi Kitabu hicho kwa Makuhani wote mmoja baada ya mwingine. wote walinunua kwa Sh. Molioni moja kila mmoja.
Makuhani kila mmoja akiwa na nakala ya kitabu hicho baada ya kukabidhiwa na RC Mongela.
RC Mongela akiwaambia neno Makuhani baada ya kuwakabidhi vitabu.
"Sasa upigwe wimbo mzuri kupongeza tukio hili", Baba Halisi akasema.
Kwaya ikipiga wimbo kama alivyotaka Baba Halisi.
"sasa baada ya hapa naenda kumwinua Rais Samia na ninyi", akasema Baba Halisi.
Baba Halisi akifanya Shukurani ya Kumwinua Rais Samia Suluhu Hassan, RC Mongela na viongozi wote ili Chanzo Halisi awainue katika utumishi wao.
Sheikh Seif na Kiongozi wa Bahai Arusha wakipokea wakati Baba Halisi akifanya Skurani hiyo ya kumuinua Rais Samia na viongozi wote. Halafu ikawa ndiyo Mwisho wa hafla👇
RC Mongela na Mwenyekiti Zelothe wakiaga tayari kwa kuondoka ukumbini.
Baba Halisi akimsindikiza RC Mongela kutoka ukumbini.
"Asante sana. Chanzo Halisi awabariki sana", akasema Baba Halisi kumwambia RC Mongela wakati wakiagana nje ya ukumbi,
Baba Halisi akaagana pia na DC Arumeru.
RC Mongela akawaaga Zelothe na DC wa Arumeru.
Sheikh akishukuru hafla ilivyofana.
Makuhani wakimfurahia Sheik wakati akipongeza.
"Haya sasa naondoka, Chanzo Halisi awabariki nyoooye mliohudhuria kila moja afike salama aendako na abarikiwe mno katika kila jambo", akasema Baba Halisi kuaga wakati akiondoka rasmi ukumbini.
Baba Halisi akisindikizwa na Kaka Huduma kutoka ukumbini. Kushoto ni Mama Halisi.
Baba Halisi akakutana na Waandishi wa habari, akazungumza nao na kuwabariki.
Kisha Baba Halisi akapanda gari lake kuondoka eneo la tukio.
©September 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇