LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 16, 2022

BUNGE SPORTS, NMB NI KIVUMBI NA JASHO KATIKA BONANZA DODOMA+video

 


 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akimkabidhi moja ya jezi Mwenyekiti wa Bunge Sports, Tarimba Abbas zitakazotumika wakati wa Bonanza la Kivumbi na Jasho litakalofanyika kesho Jumamosi Septemba 17, 2022 kwenye viwanja vya Chinangali Park na Kilimani jijini Dodoma.

Bonanza hilo linalodhaminiwa na benki hiyo litazishindanisha timu za bunge na benki ya NMB.


Zaipuna na Tarimba wakiwa pamoja na baadhi ya wabunge wakionesha jezi za Bonanza hilo.
Zaipuna, Tarimba na Ester Matiko wakiangalia fulana itakayovaliwa wakati wa matembezi kutoka eneo la Bunge hadi viwanja vya Chinangali Park.



Tarimba akizungumza na vyombo vya habari kuelezea Bonanza hilo huku akisikilizwa na Zaipuna
Zaipuna, Tarimba na wabunge wakionesha ishara ya umoja wakati wa mkutano huo na wanahabari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa bungeni Dodoma leo Septemba 16, 2022.

 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Zaipuna akikabidhi vifaa  na jezi kwa ajili ya bonanza hilo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages