LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 3, 2022

BASI LA NAJIMUNISA LAUA WATANO, KUJERUHI 54 SHINYANGA

Ibadakuli, SHINYANGA

Watu watano wamekufa na 54 kujeruhiwa katika ajali ya Basi lililogongana na Fuso  uso kwa uso eneo la Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Ajali hiyo imetokea leo Jumamosi Septemba 3, 2022  Saa 8 usiku, kwa basi la Super Najimunisa lenye usajili T.413 DAY lililokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana na Fuso lenye usajili T.123 DJH lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Dar es salaam likiwa na mzigo wa dagaa.

Manusura wa ajali hiyo Fred Mahina, amedai dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha mwendo wa kasi kubwa na kwamba walipokuwa wakimkataza aliwajibu wangetaka usafiri wa raha wangepanda ndege, huku akiwaambia wasali sana ili wafike salama.

“Tulipofika Morogoro dereva akiwa mwendokasi alikwaruza Roli tukapona kuanguka, lakini akazidi kuendesha mwendokasi abiria tulipokuwa tukipiga kelele apunguze mwendo, aligoma na kutuambia tusali, ndipo tulipofika hapa Shinyanga na kupata ajali,” anasema Mahina.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Leonard Nyandahu ambaye alikuwa eneo la ajali hiyo, amesema chanzo ni uzembe wa Dereva wa basi kwa kutozingatia vibao vya usalama Barabarani na kuendesha mwendokasi.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga Dk. Luzila John amethibitisha kupokea miili ya watu watano pamoja na majeruhi 54 ambao wanaendelea na matibabu.

Amesema miili marehemu hao bado haijatambuliwa majina yao, na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitalini hapo.
Sorce: Fullshangwe Blog


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages