LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 1, 2022

ASIYETUMIA TIKETI ZA KIELEKRONIKI FAINI LAKI 250,000

 

 Na Mwandishi wetu-Manyara  

Imeelezwa kuwa Mabasi yanayofa nya safari mikoani yataanza  kukata tiketi kwa mfumo wa mtandao kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.

Akizungumza mjini Babati wakati wa ukaguzi wa magari yanayobeba wanafunzi, Meneja mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) katika mkoa wa Manyara Joseph Michael amesema kuanzia siku ya Alhamisi septemba mosi abiria wotewatakata tiketi za kusafiria kwa njia ya mtandao (TIKETI MTANDAO).

Afisa huyo ameeleza kuwa kuanzia siku hiyo basi ambalo litakuwa halitoi tiketi ya kielektroniki halitaruhusiwa kuondoka na faini yake ni shilingi laki mbili na nusu (250,000) papo hapo.

Abiria wametakiwa kuacha kutumia tiketi zilizoandikwa kwa mkono na badala yake kutumia zinazotolewa kwenye mashine (POS) kununua wenyewe kupitia simu zao au Computer.

Mfumo wa tiketi za kielektroniki ukianza  kutumika rasmi kwa mabasi yote nchini kupitia mfumo huo,  abiria ataweza kukata tiketi na kuilipia moja kwa moja kwa njia ya mtandao bila kupitia kwa mawakala wa mabasi kama ilivyozoeleka.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages