Inaelezwea kuwa hakuna hakuna mtu aliyedhurika na moto huo japo umesababisha hasara katika kasino hiyo kwa kuteketeza vitu vyote vilivyokuwa ndani
Jeshi la zimamoto na uokoaji lilifika kwa wakati na kuanza kuuzima moto huo ili usiendelee kuleta madhara kufuatia hoteli hiyo kuwa katikati ya jiji la Mwanza na kuzungukwa na majengo mengine
Miongoni mwa waliofika katika tukio hilo ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima
Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Kamila Labani amesema wamefanikiwa kuudhibiti moto huo usisambae katika hoteli hiyo huku bado wanaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇