LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 29, 2022

WATU ZAIDI YA 12 WAUAWA NCHINI DRC

     Zaidi ya watu 12 wamepoteza maisha katika mashambulizi ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, yaliyotokea ndani ya siku tatu zilizopita. 


Kiongozi mmoja wa kijeshi katika jimbo la Kivu Kaskazini, ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema mwanajeshi mmoja aliuawa katika shambulio lililotokea kaskazini mwa mji wa Butembo na kufanywa na wanamgambo wa Mai-Mai. Aliongeza kuwa wapiganaji wawili wameuawa. 


Hapo jana, rais wa mashirika ya kiraia huko Lodjo, jimboni Ituri Prince Kaleta, alilieleza shirika la habari la AFP kuwa wachimba madini sita waliuawa kwa kukatwa vichwa na waasi wa kundi la CODECO. 


Raia wengine watatu waliuawa katika shambulio lililofanywa na waasi wa ADF usiku wa Jumamosi jimboni Kivu ya Kaskazini. Congo inakabiliana na makundi tofauti ya waasi ambayo mara nyingi huwashambulia raia.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages