Vijana 4 waliomaliza masomo ya vyuo vikuu wameamua kuanza UVUVI wa VIZIMBA
(aquaculture, fish farming) ndani ya Ziwa Victoria, eneo la Kijiji cha Bujaga, Kata ya Bulinga.
Kiongozi wa Kikundi hicho, Kijana Albert Simon ana shahada BA (Education) na amemuomba Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, awasaidie kupata msaada au mkopo wa Serikali ili wafanikishe Mradi wao wa UVUVI wa VIZIMBA, ambao ndio AJIRA yao na ajira ya vijana wengine wa Kata ya Bulinga.
Ombi.lao tayari limefikishwa Serikalini.
CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa inaonyesha matayarisho ya UVUVI wa KAMBALE utakaofanyika ndani ya Ziwa Victoria - huu ni Mradi unaongozwa na Kijana Simon Albert, Kijijini Bujaga, Kata ya Bulinga.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇