Waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamewaua takriban raia 15 na kiongozi wao wakati wa mashambulizi dhidi ya vijiji mwishoni mwa juma.Gavana wa jeshi la eneo la Ituri, Kanali Siro Simba, alisema waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) walidaiwa kushambulia kijiji cha Kandoyi Ijumaa usiku na kuwaua watu 10.
Shambulio jingine katika eneo la karibu la Bandiboli siku ya Jumamosi lilisababisha vifo vya watu watano.
Mwanamke aliyepoteza wazazi wake wote wawili alisema koo zao zilikatwa na waasi.
Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linasema kuwa lina ushahidi kwamba wanajeshi wa Rwanda wamekuwa wakipigana pamoja na kundi moja la waasi linalojulikana kwa jina la M23.
Serikali ya Kigali imekanusha shutuma hizo.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇