LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 26, 2022

CHAMA CHA WAFAMASIA CHATOA WITO KWA WAANDISHI WA HABARI KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA JAMII

 
   Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) kimetoa wito kwa waandishi wa habari nchini  kutoa elimu kwa jamii jinsi ya matumizi sahihi ya dawa ili zisilete madhara na usugu kwa wananchi.

Wito huo umetolewa na Rais wa PST Mfamasia Fadhili Hezekia alipozungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam.

"Semina hii kwa waandishi wa habari  tunalenga waweze kutumia taaluma hii ya famasi katika utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusiana na Afya hasa tabia ya matumizi holela na yasiyo sahihi ya dawa ambayo zinaleta changamoto katika maswala ya kiuchumi nchini." amesema Mfamasia Hezekia 

Pia, Hezekia ameainisha majukumu ya chama cha wafamasia ikiwa ni pamoja na kutumia weledi, fusra kwa kushiriki kuboresha huduma za upatikanaji wa bidhaa za dAfya Tanzania kwa kushirikiana na wadau kutoka nchini mbalimbali.

Katika kudhihirisha hilo amesema wameandaa maonesho ya kwanza  yanayoitwa Farmatech East Africa, katika maonesho hayo bidhaa za Afya za teknolojia za kisasa zitaoneshwa na washiriki zaidi ya 60 watashiriki katika maonesho hayo kutoka Tanzania ma nchi nyingine.

Mfamasia Hezekia amewakaribisha wataalamu,wanafunzi na wananchi   katika maonesho hayo yatakayofanyika kuanzia Augusti 30-01 Septemba 2022 jijini Dar es kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages