LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 26, 2022

VIONGOZI WA CCM, SERIKALI, DINI WAONGOZA KUMUAGA MAREHEMU KUSILA +video

Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)  wakilitoa jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma na Waziri wa  Mawasiliano na Uchukuzi, marehemu William Kusila katika Kanisa la Anglikan jijini Dodoma baada ya kufanyiwa ibada ya kuagwa tayari kwenda  kuzikwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Mtitaa, Bahi.



Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Aglikan Dodoma, Keneth Chimwaga akiongoza ibada ya kumuaga marehemu William Kusila.


Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma, Peter Mavunde akitoa salamu za rambirambi kwa marehemu Kusila.


Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo akielezea jinsi alivyokuwa karibu pamoja na kupata ushauri mbalimbali kutoka kwa marehemu Kusila.

Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wa wabunge.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi, akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya mawaziri.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, akitoa salamu za rambirambi  za mkoa huo ambao pia Kusila aliwahi kuwa Mkuu wa mkoa huo.

Katibu wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Pili Agustino akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya chama hicho.

Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Kusila wakiaga mwili wakati wa ibada hiyo.








 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, vingozi hao wakitoa salamu.....

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages