LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 6, 2022

RAIS SAMIA AONDOKA NCHINI LEO KWENDA SENEGAL, KUHUDHURIA MKUTANO WA IDA

Dar es Salaam, leo Juni 6, 2022
Rais Samia Suluhu Hassan leo ameondoka hapa Nchini kwenda nchini Senegal kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika zinazonufaika na
Dirisha la Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa), utakaofanyika kesho Julai 7, Jijini Dakar nchini humo.

Kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,  Rais Samia, ameagana na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango.

Taarifa imesema, katika mkutano huo Viongozi hao wa Nchi za Afika zinazonufaika na
Dirisha la Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa), wanatarajiwa kutoa mwito wa kuwepo kwa nguvu kubwa na umoja zaidi Katika  utekelezaji wa IDA20 unaolenga ufufuaji thabiti na ustahimilivu kwa Bara la  Afrika.

Mkutano huo unafanyika huku Nchi za Kiafrika zikiwa zimeathiriwa sana na migogoro mingi ya Kimataifa, hali ya hewa na COVID-19, viwango vinavyoongezeka vya uhaba wa chakula, na hivi karibuni zaidi na athari za vita vya Ukraine.

"Mpango wa IDA20 utasaidia kufufua uthabiti kutokana na majanga haya, na kusaidia bara kuendelea na mabadiliko yake ya kiuchumi. Mkutano huo pia utaidhinisha kazi na umuhimu wa IDA kama mshirika anayechaguliwa katika eneo hili.

IDA ni mojawapo ya vyanzo vikubwa zaidi vya fedha kwa ajili ya kupambana na umaskini uliokithiri katika nchi zenye kipato cha chini zaidi duniani. Afrika ndiyo mfaidika mkubwa zaidi wa IDA ikiwa na nchi 39 na imepiga hatua kubwa katika kuboresha viashiria vya maendeleo katika miongo sita ya ushirikiano na Benki ya Dunia mesema taarifa hiyo".

Kw mujibu wa taarifa hiyo, majadiliano ya mkutano huo yatazingatia maeneo matano ya kipaumbele kwa kanda:
(1) Mabadiliko ya Kiuchumi, (2) Kilimo, Ufugaji na usalama wa chakula, (3) Rasilimali watu,  (4) Ubunifu wa kidigitali na kiteknolojia na (5) Nishati mbadala.

"Ni muhimu sana kwa Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhudhuria mkutano huu, kwani malengo hayo matano yanayokwenda kujadiliwa yanagusa moja kwa moja mipango mkakati wa nchi yetu.

Tumuombee Afya njema Rais Samia na wote alioandamana naye katika msafara, wakaupige mwingi kama ilivyo kawaida yake Kwa maslahi makubwa ya Taifa letu", imesema taarifa hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpangokabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini dar es Salaam, tayari kwa safari ya kwendar Jijini Dakar nchini Senegal leo Julai 6, 2022 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika zinazonufaika na Dirisha la Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Leopold Sedar Senghor Jijini Dakar nchini Senegal leo Julai 6, 2022 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika zinazonufaika na Dirisha la Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages