LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 5, 2022

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KWENYE BANDA LA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KATIKA MAONESHO YA SABASABA DAR ES SALAAM

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Jenifa Omolo (Kushoto) akizungumza na Mstaafu Sura Rwiza (kulia) aliyefika kuhakikiwa Taarifa zake, katika Banda la Wizara hiyo kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (TanTrade), leo. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja.
Wanafunzi kutoka Ruangwa mkoani Lindi walipotembea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade).
Mkurugenzi wa Self Microfinance Mudith Cheyo, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Tehama Wizara ya Fedha na Mipango Zuberi Msisi, kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade).
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na  Utalii  Pro. Eliamani Sedoyeka (Kulia) akifurahia jambo baada ya kupata Elimu kutoka kwa maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (TanTrade). Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na  Utalii  Pro. Eliamani Sedoyeka (Kulia) akipokea machapisho kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Shamimu Mdee, katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (TanTrade).
Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade). Kushoto ni Afisa Mapokezi na Katibu Muhtasi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Masia Msuya.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Jenifa Omolo (aliyeshika tuzo) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) ambacho kimeibuka mshindi wa tatu katika tuzo ya jumla kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu vinavyoshiriki Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Tantrade).  Kutoka kulia ni Afisa Uhusiano wa  Chuo hicho Sarah Goroi, Afisa Uhusiano Anold Kavishe na kushoto ni Afisa Masoko Benadetha Inyasi.
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Jenifa Omolo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Takwimu Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka kulia ni Neema Madembwe Kushoto kwake ni Afisa Maktaba Mkuu Mwanaabu Ngulumbi alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (TanTrade).
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Jenifa Omolo akizungumza na Afisa Udahili wa Chuo cha Mipango ya maendeleo Vijijini (IRDP) Dk. Maclean Mwamlangala (Kushoto) kulia ni Afisa Uhusiano Stellah Masanja alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (TanTrade).

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages