LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 10, 2022

MWENYEKITI WA CCM RAIS SAMIA AOMBOLEZA KIFO CHA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA MPLA YA ANGOLA DOS SANTOS

Komredi Jose Eduardo dos Santos.
 

Dodoma, Tanzania
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salam za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama cha MPLA cha Angola na Rais wa nchi hiyo Komredi Joao Manuel Lourenco, kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho na Rais wa nchi hiyo Komredi Jose Eduardo dos Santos.

Santos ambaye amefariki dunia Ijumaa Julai 8, 2022 , akiwa na umri wa miaka 79, alitawala taifa hilo la Angola lenye utajiri wa madini, kwa takriban miongo minne, na umati umemfika katika hospitali moja katika jiji la Barcelona nchini Uhispania alikuwa akitibiwa ugonjwa ambao haujajulikana.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka hamdu Shaka, imesema, Mwenyekiti wa CCM Rais Samia amesema CCM imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Kiongozi huyo ambaye alikuwa Rais wa Pili wa Angola.

Mwenyekiti wa CCM Rais Samia, amesema Santos alikuwa mmoja wa viongozi wa kikosi kilichoshiriki ukombozi wa nchi za Bara la Afrika, wakiongoza mapambano ya mataifa ya Nchi hizo kujikomboa kutoka katika utawala wa kikoloni, na kiongozi shupavu aliyeongoza MPLA kulinda Uhuru wa Nchi yake na watu wake dhidi ya mashambulio ya wapinga Uhuru.

Amesema CCM inakumbuka na kuthamini mchango wa Komredi Santos, ambaye kwa kushirikiana na viongozi wenzake wanamapindzi wa Afrika,  miongoni mwao Rais wa kwanza wa Angola Komredi Agosptino Neto na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, waliona umuhimu wa kushirikiana kusaidia mapambano ya Uhuru wa nchi zingine zilizokua bado katika minyororo ya wakoloni, hususan nchi za Kusini mwa Afrika.

Mwenyekiti wa CCM Rais Samia, amesema, CCM itamkumbuka Komred Santos, kama kipngozi wa kuigwa aliyependa nchi yake kwa uzalendo mkubwa, ambapo kuitia uongozi wake, MPLA iliweza kusimamia Angola kuendelea kuwa taifa moja kwa maslahi ya wananchi wake.

"Mbali na kuiongoza MPLA na Jamhuri ya Angola kikamilifu katika kulinda uhuru dhidi ya matishio ya ndani na nje, Komredi Santos alishirikiana viongozi wenzake katika mapambano ya kuzikomboa nchi za Afrika Kiuchumi, Ushirikiano msingi wa kuanzishwa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), amabyo tunajivunia umuhimu wake na matunda yake wakati huu.

Kutokana na mchango wa Komredi Santos, katika harakati za ukombozi wa mataifa ya Kuisni mwa Afrika na Afrika kwa Jumla, pamoja na maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa watu katika nchi zetu, msiba huu sio wa Waangola pekee yao, bali ni wetu sote. Ni huzuni kubwa kwetu sote", amesema Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia kupitia taarifa hiyo.

Pamoja na mambo mengi aliyoifanyia Angola, Santos atakumbukwa kwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu nchini humo mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo wafuasi wake walimwita 'mbunifu wa amani'.

Akiwa amehitimu katika uhandisi wa petroli katika Umoja wa Kisovieti mwaka wa 1969, Santos alikuwa na umri wa miaka 37 tu alipokuwa Rais wa Angola muongo mmoja baadaye, kufuatia kifo cha Rais wa kwanza wa Nchi hiyo AntĂłnio Agostinho Neto.

Wakati huo, miaka minne tu baada ya kupata uhuru mwaka 1975, Angola ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi mawili yaliyokuwa yakipinga ukoloni wa Ureno ya MPLA ya Dos Santos na Unita, vita ambavyo vilidumu kwa miaka 27 na kuangamiza nchi ambapo watu 500,000 wanaaminika kufariki katika mzozo huo.

TAARIFA YA CCM HII HAPA👇

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages