LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 10, 2022

KAGAME AFIKIRIA KUGOMBEA TENA URAIS WA RWANDA 2024

Kigali, Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame (64) amesema kuwa anafikiria kugombea tena nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika mwaka 2024.


Kagame ameyasema hayo katika mahojiano maalum  na kituo cha France 24 ambapo amenukuliwa akisema “nafikiria kugombea kwa miaka mingine 20 na sina tatizo na hilo, uchaguzi unahusu watu kuchagua.”


Kagame ambaye alianza kuiongoza Rwanda akiwa na miaka 36, alibadilisha katiba ya nchi hiyo mwaka 2015 na kumruhusu kubakia madarakani hadi 2034 na katika Uchaguzi mkuu mwaka 2017 alifanikiwa kupata ushindi wa asilimia 99 ya kura.

Rais Paul Kagame

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages