LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 21, 2022

KASI YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA ELIMU, CCM YATOA NENO KWA RAIS SAMIA.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu, unaendelea kutoa matunda mazuri katika sekta hiyo na chama kinaridhishwa sana.


Shaka aliyasema hayo  (Leo) Alkhamis 21 Julai 2022 jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea maonyesho ya 17 ya vyuo vikuu yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja.


“*Maboresho makubwa yamefanywa katika sekta ya elimu, nimetembelea mabanda ya taasisi mbalimbali za elimu zinazoshiriki maonyesho haya, nimejionea na kusikia mambo makubwa ya maendeleo na kuona jinsi Rais Samia alivyopania kuleta mageuzi makubwa katika nyanja ya elimu” *•alisema.


Amefahamisha kuwa ongezeko la fedha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na wizara nzima ya elimu, ni hatua muhimu iliyotengeneza mazingira rafiki kwa sekta ya elimu ambayo ndio inayotoa muelekeo wa Taifa katika kuandaa na kuzalisha rasilimali watu watakaokuja kusukuma mbele maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini.


Kwa mujibu wa Shaka, awali kulikuwa na malalamiko mengi kuhusiasa na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambapo Chama kililazimka kukaa pamoja na Serikali (Bodi ya Mokopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu) (HESLB) ambapo kwa sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa na hali imeimarika.


“*Rais Samia amefanya kazi kubwa katika sekta ya elimu katika kipindi kifupi, moja  ya jambo ambalo  halizungumzwi  sana ni namna alivyosamehe deni la  sh. trilioni 1.1 ambalo lilikuwa halilipiki kwa bodi hii ya mikopo, hatua ambayo imefungua fursa kwa wanufaika  kuwa na uhakika wa kupanuka wigo wa kupatikana fedha na ndio maana  pia  Rais, akaongeza  fedha kwa bodi ya mikopo nchini kutoka sh 464 bilioni za awali hadi sh 570 bilioni”* alisema.


Amefafanua katika hatua ya kupigiwa mfano ni jinsi Rais Samia alivyoamua kutafuna mfupi mgumu ili kuimarisha sekta ya elimu nchini kwa kutenga bajeti ya sh. bilioni 985 mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya vikuu, kuwapatia mafunzo ya taaluma wahadhiri na kununua vitendea kazi itazidi kutengeneza mazingira mazuri kufundisha na kujifunzia hatua ambayo italeta mageuzi makubwa nchini.


Kwa mujibu wa shaka, juhudi hizo zote zinachukuliwa ni kwa ajili ya kuhakikisha rasilimali watu inayozalishwa ktika taasisi za elimu inakuwa imara na yenye kukidhi mahitaji ya wakati.


“*Azma na utayari wa Rais Samia kuibeba sekta  ya elimu sote tumekuwa mashuhuda, anaendelea vizuri sana, tunaamini uboreshaji huu utaendelea ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ibara 80 na 102 kuhusu kuimarisha utoaji wa huduma zenye ubora, viwango, manufaa na tija kwa taifa katika sekta ya elimu”* aliongezea Shaka


Awali Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), alisema wanaishukuru serikali ya CCM kwa kuendelea kuitazama kwa karibu sekta ya elimu nchini.


Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja madarakani, uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Samia katika elimu, umechochea ongezeko la wanafunzi wanaodahiliwa kwa ajili ya elimu ya juu kutoka wanafunzi 8,7934 hadi 100,620.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages