LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 24, 2022

DC MWENDA AAHIDI KUWAPELEKA MBUNGA YA TARANGIRE WALIMU WALIOFAULISHA KIDATO CHA SITA, NI BAADA YA SENSA

Na Hemedi Munga, Iramba
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amewahidi walimu wa shule ya Tumaini Sekondari kuwapeleka Mbuga ya Hifadhi Tarangire kufuatia ufaulu mzuri walioupata kidato cha sita mwaka huu.

Mwenda ametoa ahadi hiyo mwishoni mwa juma hili alipohudhuria Tamasha la Tuzo la Elimu katika shule hiyo lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule hiyo wilayani hapa.

Akiongea na walimu, watumishi wasio walimu, wanafunzi pamoja na wananchi waliohudhuria hafla hiyo fupi, Mwenda amewaasa wanafunzi kujitunza na kujilinda na vijana wanodaiwa kuwa wahuni hasa katika kipindi hichi wanachopata mapumziko mafupi ili watakaporudi watimize ndoto zao wakiwa na afya njema.

‘’ Vijana wangu tambueni kuwa Taifa linawategemea hivyo mnapokwenda mapunziko mafupi haya mjitahidi kuchukuwa tahadhari ili Taifa lipate kutoka kwenu Wahandisi, Marubani, Mameneja wa benki, Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Mawaziri na viongozi wengine.’’ Aliasa Mwenda

Aidha, aliwafunda kuacha tamaa za mwili kwa sababu ni chanzo cha kuuwa ndoto zao.

‘’ Mtaziua ndoto zenu mkiendekeza tamaa za mwili tulieni umri na muda utakapofika mtayakuta hayo mambo’’

Nasaha hizi zinakuja ikiwa ni sababu ya uwekezaji mkubwa alioufanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani katika shule hiyo.

Alibainisha Mwenda kuwa katika shule hiyo peke yake, Rais Samia ndani ya mwaka mmoja wa utawala wake, alileta takribani Tsh 1.7 bilioni.

 Fedha hizo zimekarabati na kujenga madarasa, maabara na vifaa mbalimbali ili kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia.  

Akijibu risala ya wanafunzi hao, Mwenda amewahakikishia ujenzi wa fensi kwa lengo la kuwalinda watoto wakike dhidi ya vijana wanaodaiwa kuwa sio wenye maadili mazuri, waadilifu na waaminifu atalifanyia kazi katika bajeti ya mwaka 2022/2023.

‘’ Kwa kweli mmefanya vizuri hasa kwa walimu ambao masomo yao yameingia kumi bora kimkoa na kitaifa hao nawapa ofa ya kwenda mbuga ya wanyama Tarangire wakajionee mazingira mazuri pamoja na wanyama.’’ Aliseama

Aidha, aliongeza kuwa jambo hili ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu hassan kwa sababu amekuwa akiungataza utalii ndani na nje ya mipaka ya Taifa letu.

Akisoma taarifa fupi ya shule hiyo mbele ya Mkuu huyo wa wilaya Mkuu wa shule hiyo, Zainabu Mtinda aliwataka wanafunzi hao kumshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufika shuleni hapo.

‘’ Hapa Tumaini Sekondari ni sehemu salama na nzuri ya nyinyi kufikia malengo yenu mazuri, hivyo ninawaombea afya njema ili muweze kutimiza ndoto zetu na kuzinufaisha jamii.’’

Akiongea na wanafunzi hao Afisa Elimu Taaluma wilaya hiyo, Patricia Ngaa aliwataka wakuu wa Shule wilayani hapo kuiga mfano wa Siku ya Elimu Tumaini Sekondari.

Aidha,aliwapongeza walimu hao kwa namna ambavyo wamekuwa wakikuza taaluma na kufanikisha kufaulisha wanafunzi kwa daraja lakwanza, lapilli na latatu.

‘’ Napenda kuwapongeza kwa matokeo mazuri ya kidato cha sita mwaka 2022, hongereni sana kwa kweli mmejitahidi!’’ alipongeza Ngaa na kuongeza kuwa

‘’ Tunajivunia Tumaini Sekondari imekuwa shule ya mfano kwa ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa kwa matokeo bora.’’

Kwa upande wake mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule hiyo, Neema Jackson alisema kuwa wamesherehekea siku ya Elimu Tumaini Sekondari kwa sababu katika miaka mitatu shule hiyo imekuwa ikipata ufaulu mzuri katika vidato vyote pamoja na kupata miundominu bora.

Naye mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, Yustra Hamisi alisema kuwa wanafurahia siku hiyo kwa sababu wanaonesha vipaji vyao na njia za kujifunzia wanazozipata toka kwa walimu wao mahiri na wabozi wa taaluma.

Tumaini Sekondari ni moja kati ya shule kongwe wilayani Iramba mkoani Singida ambayo ilianzishwa mwaka 1969. Kwa sasa ni shule inayodahili wanafunzi wa jinsia ya kike tu kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda akitoa zawadi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika hafla ya  siku ya Elimu, Shule ya Sekondari Tumaini, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule hiyo jana Julai 23, 2022. (Picha na Hemedi Munga)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages