LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 13, 2022

CHONGOLO AWAPA THAMANI, HESHIMA KUBWA MABALOZI WA CCM WA MASHINA+video

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesema kuwa kwa CCM mabalozi wa Mashina wana thamani isiyoelezeka wala haina mjadala ni wenye heshima kubwa na ndiyo maana wamepewa mamlaka ya kupeperusha bendera saa 24 kuliko hata viongozi wa ngazi ya juu. Ameyasema hayo muda mfupi kabla ya kuwagawia bendera wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa mashina na matawi waliochaguliwa hivi karibuni mkoani Dodoma. Mafunzo hayo ameyafungua leo Julai 13, 2022 kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambapo wamefundishwa kuhusu itikadi, elimu ya sensa na ulinzi na usalama.




 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Chongolo akiwapongeza na kuwapa thamani mabalozi wama mashina.....

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages