LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 27, 2022

BALOZI FATMA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA UJUMBE WA SERIKALI YA OMAN, JIJINI DODOMA

Dodoma, Tanzania

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab amekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Serikali ya Oman leo tarehe 26 Julai 2022 katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Oman kwakuwa nchi hizo zinashirikiana katika sekta za biashara, kilimo, uwekezaji, utalii, afya, elimu, ujenzi wa miundombinu,madini na uvuvi.

Ujumbe huo upo nchini kwa ziara ya siku 6 na unaongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje wa Oman, Mhe. Mohammed Bin Nasser Al Wahaibi ambaye ameambana na viongozi wengine wa Serikali ya Oman.

Pamoja na Balozi Fatma Rajab, ujumbe huo pia umefanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Antony Mtaka pamoja na uongozi wa jiji la Dodoma ambapo, ulipata wasaa wa kutembelea kiwanja kilichotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kujenga ofisi za Ubalozi wa Oman.

Aidha, tarehe 25 Julai 2022 ujumbe huo ulikutana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo ulifanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Ziara ya ujumbe huu ni matokeo ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Oman.

Hivyo, ujumbe huu upo nchini kufanya ufuatiliaji wa masuala ya utekelezaji katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano yaliyokubaliwa wakati wa ziara hiyo na kuangalia namna ya kuhuisha mikutano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akizungumza na Katibu Mkuu Mambo ya Nje wa Oman, Mhe. Mohammed Bin Nasser Al Wahaibi jna, Julai 26, 2022 katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Naibu Kkatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab alipokuwa akisalimiana na ujumbe wa Serikali ya Oman uliopomtembelea katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma. Ujumbe huo umeongozwa na Katibu Mkuu Wiazara ya Mambo ya Nje wa Oman, Mhe. Mohammed Bin Nasser Al Wahaibi

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages