LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 27, 2022

MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KIISLAMU WA 1444 KUFANYIKA ZANZIBAR JULAI 31, MWAKA HUU

Na Rahma Khamis, Maelezo Zanzibar
Kongamano la kudhimisha mwaka mpya wa Kiislamu wa 1444  litafanyika Julai 31, 2022, (Mwezi Muharram 1444) katika Msikiti wa Jamiiu Zinjibar Mazizini, Zanzibar, huku ukitolewa mwito kwa Waislam wote kushiriki katika Kongamano hilo.

"Waislamu walio wengi siku hizi hawafahamu mwaka mpya wa Kiislamu jambo ambalo litasababisha kizazi kijacho kukosa kufahamu dini yao, hivyo kufanyika kwa kongamano hilo kutasaidia kufahamu mambo mengi yanayohusiana na uislamu", amesema, Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume wakati akizungumza Ofisini kwake Mazizini, kuhusu maadhimisho hayo.

Katibu huyo amesema , katika kongamano hilo mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo Hijra na Sensa ambayo itawasilishwa na Shekh Khamis Abdulhamid, Mtume kuhama Makka kuhamia Madina ambayo itawasilishwa na Shekh Othman Maalim na Umuhimu wa elimu ambayo itawasilishwa na Sheikh Shaaban Batash Mjumbe wa Baraza la Ulamaa.

Amesema ni vizuri Waislamu kujua lengo la Uislamu na kuikumbusha jamii ili kuwa na tabia njema kwani unahimiza umoja, mshikamano , amani na heshima hivyo ipo haja kujitahidi ili kwenda sanjari na uislamu.

Amesema  kufuatia maadhimisho hayo ya mwaka mpya w Kiislam mwezi Muharram, Ofisi ya Mufti imeona ipo haja ya kufanya shamrashara kuelekea siku hiyo ambapo kutafanyika mambo mbali mbali ikiwemo uchangiaji wa damu salama katika Mnara wa Kisonge.

Pia amefafanua kwamba kutakua na uzinduzi wa Baraza la Maulid katika Ukumbi wa Shekh Idrissa Abdulwakili sanjai na dhwafa itakayoanzia Msikiti wa Muembe Shauri na kumalizikia Bwawani.

Aliongeza kwa kesema kuwa tarehe 30 mwezi huu kutakua na ziara ya kutembelaea wagonjwa katika Hospitali ya mnazimmoja ili kudumisha umoja na mshikamano wa waislamu Nchini.

”Katika sherehe zetu tumeamua kufanya hivi ili waislamu wajue kwamba ni dini yenye kuhimizana watu kutendeana mambo mema katika jamii kwani tukifanya hivi wagonjwa watapata faraja kuona kuwa wanatembelewa na kujulikana halizao,”alisema Katibu Mfaume.

Katibu wa Mufti Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume akizungumza na Waandishi wa Vyombo mbalimbali Habari wa kuhusiana na maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislamu wa 1444, Ofisni kwake Mazizini Zanzibar, jana. (Picha na Fuzia Mussa, Maelezo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages