LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 7, 2022

WAZIRI UMMY AWASILI NCHINI UFARANSA KUHUDHURIA MKUTANO WA GFF

 
     Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,leo tarehe 6 Juni, 2022 amewasili katika Jiji la Paris , Ufaransa kuhudhuria kikao cha Jumuia ya Wafadhili wa Huduma za Afya ya Mama na Mtoto (Global Financing Facility - GFF).

Akiwa nchini Ufaransa Waziri Ummy amekutana na Mawaziri wenzake kutoka Sierra Leone, Bukinafaso, Niger  na nchini nyingine kwenye kikao cha kuzungumzia changamoto zinazokwamisha katika utoaji huduma bora.

Akizungumza kwenye kikao hicho Waziri Ummy amesema upungufu wa watoa huduma wenye ujuzi ni changamoto kubwa inayoikabili Tanzania katika kuhakikisha inatoa huduma bora. 

Aidha, ubora wa mafunzo yanayotolewa na kile wanachokipata wahitimu ametaja kuwa ni  tatizo linalochangia kwenye matokeo yasiyotarajiwa kwenye vituo vya kutolea huduma.

Ameongeza kuwa Tanzania ina shida kwenye kutumia watoa huduma ngazi ya jamii wakati uzalishaji wa watoa huduma wenye ujuzi likiwa kubwa. Swali linagonga vichwa ni je "tumchukue asie na ujuzi au mwenye ujuzi" ili kuweza kupata matokeo yenye tija zaidi

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages