Kinamama wakigalagala kuonyesha heshima na furaha yao kwa ujio wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka aliyewasili wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi kwa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Uhai wa Chama.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akicheza na vijana wa hamasa baada ya kupokelewa katika Kijiji Cha Mandawa, Kata ya Mandawa alipowasili wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi kwa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Uhai wa Chama.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akipiga Ngoma ya. ligongo baada ya kupokelewa na kushiriki ujenzi wa jengo la Zahanati ya Kijiji cha Chikundi, Kata ya Chikundi alipowasili wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi kwa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Uhai wa Chama.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akishiriki ujenzi wa jengo la kituo cha Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi alipowasili mjini humo kwa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Uhai wa Chama.
****************************
Na Mwandishi Maalum, Ruangwa
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa {NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema Rais Samia Suluhu Hassan sasa anakirejesha Chama kwenye zama za ujamaa na kujitegemea kama ilivyoasisiwa na viongozi wa taifa wakiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.
Shaka aliyasema hayo leo aliposhiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Namichiga, katika Halmashauri ya Wilaya ya, Ruangwa akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Lindi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na uhai wa Chama ambapo alieleza kufutahishwa kwake na ushiriki wa wananchi katika ujenzi huo kwa kujitolea.
“Mwenye kokoto, mwenye simenti, mwenye kila kitu tunakwenda kuunga nguvu ujenzi wa taifa ili kufikia maendeleo kwani hatuna mjomba, hatuna shangazi, hatuna mama mdogo atakayetoka anakotoka aje atufanyie kazi ya kujenga maendeleo kwa umoja wetu, mchango wetu ni muhimu ili Chama hiki kuhakikisha kimesimama.
“Wazee wetu walifanya haya tunayoyafanya sisi (kujitolea nguvu). Nimefarijika sana na kinamama mnavyotisha katika kushika hatamu za kuongoza nchi kama ambavyo Rais Samia anafanya, lakini mnatisha kwenye kuhamasisha maendeleo.
“Wakinamama kwenye ujenzi wamekuwa wengi zaidi, kwenye uhamasishaji wamekuwa wengi zaidi, kwenye kutuongoza wanafanya vizuri zaidi kama anavyofanya Rais Samia, Mungu awabariki sana, Mungu awalinde sana mama zetu kwa namna ambavyo mnaleta ari na shine kwenye taifa hili,” anasema.
KASI YA MAENDELEO PALEPALE
Awali akizungumza kwa nyakati na maeneo tofauti baada ya kupokeleewa na wananchi katika Kijiji cha Mandawa, wilayani humo, Shaka alisema serikali chini ya Rais Samia itaendelea kuleta maendeleo kwa kasi.
Shaka alisema kutokana na kutambua mchango wa wakulima serikali ya awamu ya sita itaendelea kutatua changamoto za wananchi.
Alisema anatambua kuwa huko nyuma kulikuwa na changamoto katika kilimo cha zao la korosho, lakini serikali chini ya Rais Samia imeendelea kuzitafia ufumbuzi.
Kwa mujibu wa Shaka, miongoni mwa utatuzi wa changamoto ni pamoja na kutoa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima wa korosho ambazo zitagawiwa bure kwa wakulima wa zao hilo.
“Nipongeze mpango wa serikali wa kutoa pembejeo bure kwa wakulima, Rais Samia anafanya maendeleo bila kubagua na bahati nzuri Mbunge wenu (Wazi Mkuu, Kassim Majaliwa) naye anafanya kazi nzuri ya kuhakikisha anawatetea wananchi wa Ruangwa.
“Serikali ya Rais Samia itaendelea kutatua changamoto na kuleta maendeleo. Tumeelezwa hapa kuwa Wilaya ya Ruangwa huko nyuma walikuwa wanapata sh million 400 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, lakini chini ya Rais Samia wamepokea zaidi ya sh. bilioni 1.5,” alisema.
Akizungumza mbele ya Shaka baada ya kukaribishwa ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali ya wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma alisema serikali ya awamu ya sita imeendelea kutatua changamoto ikiwemo ya ufikishaji wa pembejeo kwa wananchi kwa wakati.
“Kwenye pembejeo Rais amedhamiria kugawa pembejeo bure na tayari zimefika na Rais ameamua mwaka huu wagawe wananchi wenyewe, huko nyuma kulikuwa na ujanjaujanja, hadi wiki ijayo zitakuwa zimewafikia.
Kuhusu hoja ya wananchi kuomba mikopo kwenye Taasisi za fedha, Ngoma alisema mazungumzo yanaendelea kuona namna nzuri ya wakulima kupata mikopo na kuirejesha kwani moja ya malalamiko ya taasisi za fedha kuwa wanaochukua fedha hawarudishi baada ya mavuno kwa kufanya ujanjaujanja ikiwemo kubadilisha majina.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇