Meneja Mradi wa Reli ya Kisasa ya Umeme SGR -TRC Mhandisi Machibya Masanja akiwatambulisha wakandarasi wa mradi huo Kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo wakati alipowasili ktika eneo la ujenzi kijiji Cha Malampaka Maswa mkoani Simiyu kipande Cha Isaka Mwanza wakati alipokagus mradi huo akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2020-2025 na uhai wa chama.
Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Mbunge wa Maswa Magharibi na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Ndaki wakati alipowasili katika eneo la mradi kwenye eneo la ujenzi Kijiji Cha Malampaka kushoto ni Mh. Stanslaus Nyongo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki.
Wahandisi wa Kampuni ya CCCC wanaojenga kipande Cha Isaka -Mwanza wakimsubiri Katibu Mkuu wa CCM ndugu Daniel Chongolo.
Mafundi wakendelea na kazi ya ujenzi wa madaraja madogo ya reli hiyo.
……………………………………
Meneja wa Mradi wa Reli ya (SGR) amesema utekelezaji wa mradi huo katika awamu ya kwanza, kipande cha kwanza wamefikia asilimia 96.3 ya utekelezaji na wameshaanza majaribio kwa kuingiza umeme katika mfumo wa uendeshaji.
Mhandisi Masanja ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kipande Cha Isaka -Mwanza Kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo wakati alipokagua mradi akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu.
“Tunategemea mpaka Juni 8 mwaka huu, tutakuwa tumekamilisha vituo vyote vya umeme vya kupozea, na tumeunganisha kutoka station ya Dar es Salaam mpaka Morogoro na tunaanza kufanya majaribio,” amesema Masanja.
Ameongeza kuwa kipande cha pili wako asilimia 85 kutoka Morogoro hadi Makutopola Singida, na alibainisha kwamba kutokana na kuchelewa Kwa asilimia 0.4 kukamilisha moja ya eneo, lakini wanampango kazi walio waliojiwekea itakapofika Juni wawe wamefikia asilimia kadhaa.
Amewataka wakandarasi kusimamia mradi huo wa SGR kuhakikisha unaleta matokeo yaliyokusudiwa.
Akizungumza baada ya ukaguzi wa mradi huo, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo amesema mkandarasi wa mradi waongeze Kasi ya utekelezaji Ili kumaliza mapema na kwa wakati na kuondoa gharama ambazo zinaweza kuongezeka iwapo mradi huo utachelewa kumalizika.
Katika hatua nyingine Chongolo amepongeza kampuni Kampuni ya uhandisi ya China (CCECC) Kwa kuoa Shilingi bilioni1 itakayotumia kufufua majengo ya Matongo mkoani Simiyu na kuyaboresha kuwa Shule ya Sekondari ya wasichana
Amesema kuanzishwa kwa chuo hicho katika eneo hilo kutasaidia kuwanufaisha wafugaji wa mkoa huo na shughuli wanazofanya.
“Kuwepo chuo hiki kutabadili na kuboresha maisha ya wafugaji kutoka ufugaji wa kienyeji na kwenda kisasa” amesema.
Pia Chongolo, amesema kwa kuwa miradi hiyo hutumia gharama kubwa kutekelezwa, ni vema wananchi wa eneo husika waone tija ya utekelezwaji wake.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ametoa taarifa Kwa Katibu mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo kuwa mkandarasi wa mradi huo kampuni ya uhandisi ya China (CCECC) imeridhia kutoa fedha hizo shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kufufua majengo hayo.
Amesema majengo hayo yalitekelezwa yalikuwa porini hayakuwa yanatumika. Kamati ya Siasa ndiyo iliyaibua na tukashauriana na kutafuta wafadhili tumempata CCECC aliyeahidi kutoa Sh1 bilioni,” amesema.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇