Mbunge wa Busanda, Tumaini Magessa ameishauri serikali kutoa elimu kwa wananchi kabla haujaanza utaratibu wa kila mtu kupatiwa namba ya utambulisho (TIN NUMBER) ili jamii ipate uelewa juu la hilo.
Aidha, Magessa ameshauri serikali kujikita kupeleka umeme maeneo ya machimbo na viwandani ili kuongeza uzalishaji. Pia imemshangaza kwenye bajeti kuonesha kwamba Ranchi ya Taifa ya Kongwa badala ya kuiboresha inadhoofishwa kwa baadhi ya eneo lake kumegwa kwa ajili ya kilimo. Ametoa ushauri wake huo alipokuwa akitoa maoni yake wakati wa mjadala wa Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali bungeni Dodoma Juni 17, 2022.Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Magessa akitoa ushauri wake huo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇