LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 19, 2022

KAPUFI AIPONGEZA SERIKALI KUACHA KUWAADHIBU WANANCHI BADALA YAKE KUANZA KUWAADHIBU WALIOSABABISHA HATI CHAFU+video

 


 Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi ameiomba serikali kupeleka wataalamu wa utafiti kutoka GST kusaidia wachimbaji wadogo wa madini kwenye maeneo yao ya machimbo ili kuboresha sekta hiyo.

Aidha, ameipongeza Serikali kurekebisha utaratibu wa zamani wa kuwaadhibu wananchi kwa kuwanyima huduma kutokana na hati chafu ya halmashauri na badala yake itakuwa inawaadhibu watakaosababisha. Lakini vilelvile kutochezea zawadi tuliyopewa na Mungu ya hifadhi za Ngorongoro na Serengeti ama sivyo tutapatiwa laana. Kapufi ametoa ushauri wake huo, alipokuwa akitoa maoni yake katika mjadala wa mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali bungeni Dodoma Juni 17, 2022 bungeni Dodoma.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Kapufi akitoa ushauri wake huo....
 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages