LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 2, 2022

KATIBU MKUU WA CCM CHONGOLO ALAKIWA ITILIMA



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Itilima Bw. Hassan Milanga mara baada ya kupokelewa katika kata ya Nkoma Itilima  Leo ,  Chongolo anaendelea na Ziara yake Mkoa wa ambapo  amewasisitizia Wizara ya Maliasili na Utalii kushughulikia changomoto ya Tembo kuharibu mazao ya wakulima pamoja na makazi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Combred Daniel Chongolo  akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Itilima akiwa katika Ziara yake Mkoa wa Simiyu kwa kupokelewa Wilayani Itilima kata ya Nkoma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Combred Daniel Chongolo  akisalimiana  na viongozi mbalimblai akiwa kwenye Ziara yake Mkoa wa Simiyu kwa kupokelewa Wilayani Itilima kata ya Nkoma.

 

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Meatu akimuaga Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo mara baada ya kumaliza ziara yake wilayani Meatu na kuanza wilaya ya Itilima Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohammed na wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Itilima Faidha Salim.

 

…………………………………

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amemtaka mbunge wa Jimbo la Itilima Njelu Silanga kuwawezesha wakulima wa Jimbo Hilo kuhakikisha Kila tarafa wanapata Mashine ya kukamua mafuta ya alizeti Ili kuongeza thamani ya zao hilo ambapo kwa Mkoa wa Simiyu, Itilima inaongoza kwa uzalishaji wa alizeti.

“Najua Mbunge wenu ana wajibu wa kuwasaidia mashine za kuchuja mafuta ya alizeti, wasaidie wananchi Hawa wapate mashine za kuchuja mafuta ya alizeti angalau kwa mashine moja kwa Kila tarafa na hili litawasaidia sana kuongeza thamani ya zao hili.”

Katibu Mkuu ameongeza kuwa kitendo Cha kufunga mashine, wakulima wataanza kuuza mafuta badala ya kuuza alizeti zenyewe, ambapo kwa sasa mafuta ya alizeti ndio mafuta bora na ghali zaidi, hivyo wananchi watapata fedha za kutosha tofauti na sasa.

Chongolo ameyasema hayo leo tarehe 2 Juni, 2022 alipowasili Wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu wakati akiendelea na ziara yake yenye lengo la kukahamasisha uhai wa Chama ngazi za mashina na Kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.










No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages