LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 23, 2022

HII HAPA HATMA YA KINA MDEE BAADA YA KESI YAO KUTUPILIWA MBALI NA MAHAKAMA JANA

Na CCM Blog
Jana Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, ilitupilia mbali kesi ya msingi iliyofunguliwa na Wabunge 19 wa viti maalum Chadema ya kupinga kuvuliwa uanachama na chama hicho.

Ilielezwa kwamba, Mahakama Kuu ilitupilia mbali maombi ya msingi ya Wabunge hao kutaka kupewa kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama na kwamba sababu iliyofanya Mahakama kuchukua uamuzi huo ni kwamba maombi hayo yalikosewa kwa jina la mjibu maombi namba moja ambaye ni Bodi ya Wadhamini ya Chadema.

Sasa, bila shaka wapo watu wengi hasa wadadisi wa mambo ya siasa ambao wanajiluza au kuulizana kwamba je, kwa uamuzi huo ulitolewa na Mahakama Kuu, ndiyo mwisho wa hatma ya Wabunge hao 19 akiwemo Halima Mdee na mwenzake Ester Bulaya?

Hebu tusome tafakuri ya Mwanasheria mmoja (hakutaja jina lake) ambaye ameeleza kwa kiasi chake nini hasa inaweza kuwa hatma ya wabunge hao kulingana na sababu zilizoikifikisha Mahakama kutupilia mbali kesi yao.

Mwanasheria huyo anasema; "Maombi ama Kesi inaweza kutupwa na mahakama kwa namna moja kati ya mbili.
Inaweza kutupwa katika namna ambayo huwezi kuirudisha tena/kuifungua upya, ama inaweza kutupwa katika namna ambayo unaweza kuirudisha tena/ kuifungua upya.

Kutupwa katika namna ambayo unaweza kuirudisha tena kitaalam huitwa 'STRUCK OUT' ,  wakati ile ambayo huwezi kuirudisha tena hutwa kitaalam 'DISMISSAL', 'STRUCK OUT' maana yake kuna kitu kimekosewa ambacho kikirekebishwa kesi inarudishwa/kufunguliwa upya.

Kesi ya kina Mdee imetupwa katika namna ambayo inaweza kurudishwa tena/kufunguliwa upya 'STRUCK OUT'.
Sasa kwa kesi ya msingi ya uhalali wao bungeni haikusikilizwa hata kidogo, bali mahakama imesikiliza makosa ya kiufundi na ikaamue iitupe kabla ya kusikiliza kesi ya msingi ili wahusika wakayarekebishe hayo makosa wairudishe tena ama waachane nayo, uamuzi ni wao.

Aghalabu,  namna ya kuirudisha ni kuwa kama umejiandaa inaweza kutupwa na muda huohuo hata kabla watu hawajatoka mahakamani au wakingali bado wanashangilia ukairudisha kwa kufungua nyingine hapohapo.

Ni kurekebisha tu makosa na kuanza upya. Isipokuwa yale mazuio unayokuwa umepata yanakufa na ile iliyotupwa na hivyo huu muda wa katikati ambao hujafungua nyingine unakuwa haupo salama kwakuwa huna zuio lolote linalokulinda na hivyo lolote  laweza kufanyika dhidi yako, hivyo la kufanya ni ufungue upya haraka na uombe zuio jingine jipya haraka kabla hujapata madhara ya kutokuwa na zuio.

Kwa msingi huu Kina Mdee bado wanayo nafasi kwa kufungua upya kesi yao Mahakamani wakati wowote ikiwa watapenda kufanya hivyo na pia wafungue upya tena kuomba zuio jingine jipya haraka kabla hawajapata madhara ya kutokuwa na zuio.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages