Na Rabia Nandonde, CCM Blog Mbinga
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo amesifu namna uchimbaji na uchakataji wa makaa ya mawe unavyofanyika kwa kiwango bora ambacho kina kidhi mahitaji ya soko la ndani na nje.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika migodi ya makaa ya mawe ya Ruvuma mine coal na Jitegemee mine coal kwaajili ya Kupokea taarifa ya uchimbaji wa makaa ya mawe ambapo alisema hadi sasa tayari usafirishaji wa makaa hayo umefikia katika nchi mbalimbali za Senegal, Misri, Kenya, uganda na Malawi, na sasa wameanza kusafirisha kwenda nchi nyingine za bara la Ulaya.
“Ni wapongeza wachimbaji wa makaa yam awe pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya wakiambata na Afisa madini walifanya ziara ya kutembelea migodi ya makaa ya mawe ambayo ni Ruvuma mine coal na Jitegemee mine coal”
“Nimetembelea eneo hili ili kupokea taarifa ya uchimbaji wa makaa ya mawe kwa migodi hii kutoka kwa Ruvuma mine coal na Jitegemee mine coal ili kujua namna shughuli za uchimbaji, uchakataji na mauzo/usafirishaji zinavyofanyika katika migodi hayo” alisema Mangosongo
“Nitoe onyo kwa madereva pamoja na wafanyakazi wengine acheni kumwaga makaa ya mawe barabarani wakati wa usafirishaji pia zingatieni mwendo unaofaa sio mkali na usiofaa kwa madereva lakini naambiwa hapa pia kuna vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake vinavyofanywa na madereva yeyote atakaedhibitika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake acheni kuwarubuni na kuwakatili wanawake”
“Nawakaribisha wawekezji kuja kuwekeza katika Wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma na Nchini kwaujumla kwasababu mazingira ya uwekezaji ni rafiki na salama kwa uwekezaji hasa Wilaya ya Mbinga” alisema Mangosongo
Your Ad Spot
Jun 19, 2022
Home
featured
Uchumi
DC NANDONDE ASIFU UCHIMBAJI NA UCHAKATAJI MAKAA YA MAWE UNAVYOFANYIKA KWA KIWANGO BORA
DC NANDONDE ASIFU UCHIMBAJI NA UCHAKATAJI MAKAA YA MAWE UNAVYOFANYIKA KWA KIWANGO BORA
Tags
featured#
Uchumi#
Share This
About Bashir Nkoromo
Uchumi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇